Home Habari za Simba Leo NYIE HANGIKENI TU…LAMECK LAWI HUYOO KATUA ULAYA

NYIE HANGIKENI TU…LAMECK LAWI HUYOO KATUA ULAYA

Habari za Simba- Lameck Lawi

Huku sakata lake likiwa bado halijaamuliwa, mchezaji ambaye amezua sintofahamu kati ya Simba na Coastal Union, Lameck Lawi, muda wowote kuanzia sasa anatarajiwa kuelekea nchini Ubelgiji kwa masuala yake binafsi, imeelezwa.

Simba ilipeleka shauri lake kwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), kuhusu kuvunjiwa mkataba na Coastal Union wa kumsajili beki Lawi kungali walishafanya biashara na kukamilisha malipo, lakini wauzaji wa mchezaji huyo wakazirejesha wakidai malipo yalifanywa baada ya muda wa makubaliano kupita.

Hata hivyo, shauri hilo lilisikilizwa Jumanne wiki hii, kwa pande zote kutoa vielelezo, lakini bado halijatolewa uamuzi wa nani hasa anapaswa kummiliki mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa Nipashe Msemaji wa Coastal Union, Abbas El Sabri, alisema baada ya kurejea Tanga mchezaji huyo aliomba ruhusa ya wiki moja kwa ajili ya safari yake ya Ubelgiji.

“Kwa sasa Lameck hayupo kambini ameomba ruhusa ya wiki moja kuelekea nchini humo, kwa mujibu wa ruhusa yake anatakiwa awapo kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Agosti 8, mwaka huu, dhidi ya Azam FC,” alisema El Sabri.

Alisema kwa sasa wanasubiri maamuzi yatolewe na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kutokana na sakata la mchezaji wao huyo dhidi ya Simba.

Je Simba watakubal kumuachiamchezaji huyo? Fuatilia Taarifa zetu  kwa uhakika wa Habari.

SOMA NA HII  WAKATI MASHABIKI WAKISUBIRI 'THANK YOU' YA ONYANGO...AHMED ALLY KAAANIKA JAMBO LILIVYO...