Home Habari za Simba Leo MAMELODI SUNDOWN WAINGILIA DILI LA MCHEZAJI WA SIMBA

MAMELODI SUNDOWN WAINGILIA DILI LA MCHEZAJI WA SIMBA

habari za simba- Fei Toto

SIMBA SC ni moja kati ya Vilabu vilivyopiga hodi mitaa ya Chamanzi kuulizia uwezekana wa kuipata saini ya Kiungo wao Feisal Salum “Fei Toto”.

Mnyama alifanya mazungumzo na Azam FC kuhusiana kumsajili kwa mkataba wa kudumu Fei Toto, ili kuongeza nguvu katika kikosi chao.

Simba walikuwa wanaamini kabisa wakimpata Zanzibar Finest, basi ugonjwa wa timu yao kushindwa kutengeneza nafasi nyingi za mabao na kufunga litakuwa limekwisha.

Lakini jambo lililokwamisha usajili huo inatajwa kuwa ni moja kati ya kipengele kilichopo kwenye mkataba wa Azam FC na Fei Toto kutoka Yanga.

Yanga waliwauzia Fei Toto kwa makubaliano ya kwanza endapo wakitaka kumuuza basi wapatiwe taarifa, na timu itakayomnunua basi itailipa yanga kiasi cha Takribani Bilioni Moja.

Habari sasa zimebadilika na Miamba ya Afrika ya Kusini imeingia Sokoni kwa kutuma ofa ya pili baada ya kwanza kukataliwa.

Taarifa inasema kwamba “Klabu ya Mamelodi Sundowns imepanga kutuma ofa ya pili kwa klabu ya Azam kwa ajili ya huduma ya Feisal Salum. Sundowns wanataka kuziba pengo la Bongani Zungu na Gaston Sirino ambao wametimka klabuni hapo.

“Kwa mujibu wa tovuti ya Soccer Laduma (SNL), ofa ya kwanza ya Rand milioni 25 (TZS bilipni 3.7) ilikataliwa na mabosi wa Azam, na sasa wameandaa Rand milioni 32 (TZS bilioni 4.7) ili kupata huduma za kiungo huyo.

“Inaripotiwa kuwa mazungumzo kati ya Azam na Mamelodi hayakusimama tangu ofa ya kwanza, lakini Azam wanahitaji angalau Rand milioni 36 (TZS bilioni 5.2) ili kumuachia Fei Toto.

“Msimu uliopita wa 2023/24, Fei Toto alimaliza ligi akiwa na magoli 19 nyuma ya Aziz Ki aliyepachika nyavuni mabao 21. Hivi sasa yupo Morocco wakijiandaa na msimu mpya wa mashindano na tayari amefunga magoli 2 kwenye mechi moja ya kirafiki dhidi ya Zimamoto ya Zanzibar.”

SOMA NA HII  BAADA YA MASHABIKI KUUPONDA USAJILI WAKE....IVO MAPUNDA AIBUKA NA UJUMBE HUU KWA KYOMBO...AMTAJA GEORGE MPOLE...