Home Habari za Yanga Leo SABABU YA YANGA KUSHINDA 4-0 SAUZI NI HII.

SABABU YA YANGA KUSHINDA 4-0 SAUZI NI HII.

habari za yanga leo-AZIZ KI

USHINDI MNONO wa mabao 4-0 waliopata Yanga vs Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini unawapa taji la kwanza la Toyota Cup 2024 huku wakiweka wazi kuwa siri ya ushindi huo ni kuona kila kitu ni muhimu kwao kushinda ndani ya uwanja.

Ikumbukwe kwamba Kaizer Chiefs inanolewa na Nasreddine Nabi ambaye aliwahi kuifundisha Yanga kabla ya mikoba yake kuchukuliwa na Miguel Gamondi ambaye alikuwa kwenye benchi la ufundi Julai 28 2024 wakati wakitwaa taji hilo la kwanza ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2024/25.

Kwenye mchezo huo mabao ya Yanga yamefungwa na Prince Dube dakika ya 25, Aziz Ki ambaye alifunga mabao mawili ilikuwa dakika ya 45, 63 na Clement Mzize dakika ya 57.

Clatous Chama kiungo mshambuliaji wa Yanga ambaye ni ingizo jipya akitokea Simba alipokuwa kwa msimu wa 2023/24 ameweka wazi kuwa ni furaha kwao kupata ushindi na malengo ni kupata makombe zaidi wanayoshindania.

“Kwetu sisi kila kitu tunachukulia kwa umuhimu mkubwa hivyo ushindi wetu na kupata kombe hili ni muhimu. Tunaamini ni mwanzo mzuri hivyo tutazidi kupambana kufanya vizuri kwenye mechi zetu zote mashabiki wazidi kujitokeza uwanjani kushuhudia burudani zaidi.”

Yanga inatarajiwa kurejea Dar kwa ajili ya mwendelezo wa maandalizi ya msimu wa 2024/25 ambapo Agosti 4 2024 inatarajiwa kuwa Wiki ya Mwananchi siku ambayo watafanya utambulisho wa wachezaji wapya na wale ambao walikuwa kwenye kikosi msimu wa 2023/24.

SOMA NA HII  YANGA ITAFIKA FAINALI CAF...GAMONDI AFUNGUKA