Home Habari za Yanga Leo YANGA KUTUA LEO ALFAJIRI NA KOMBE

YANGA KUTUA LEO ALFAJIRI NA KOMBE

Habari za Yanga Leo

BAADA ya kutwaa taji la Toyota Cup Afrika Kusini Mabingwa mara 30 wa Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga kinatarajia kuwasili alfajiri ya kesho.

Yanga imetwaa taji hilo baada ya kuifunga Kaizer Chiefs mabao 4-0 mchezo wa kimataifa wa kirafiki kwa timu zote mbili ambazo zinajiandaa na ligi na michuano ya kimataifa.

Akizungumza na wanahabari, Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amewaita mashabiki wao kujitokeza kwa wingi kuwapokea wachezaji ambao watawasili nchini sasa tisa alfajiri kuamkia kesho.

“Kuanzia saa saba usiku Wananchi mnatakiwa kuanza kujitokeza kwa wingi kuwapokea mashujaa wetu ambao wametwaa kombe ugenini,” amesema na kuongeza:

“Timu ikiwasili itaruhusiwa kuondoka kwenda kupumzika, lakini kombe tutabaki nalo na kutoka nalo uwanja wa ndege hadi makao makuu Jangwani kwa ajili ya kulihifadhi.”

Naye Afisa Uhamsishaji wa Yanga, Haji Manara amesema Yanga imejitengenezea ubora na inaonyesha ukubwa wake kutokana na ubora wa kikosi ilicho nacho.

“Yanga imejitengenezea ubora na anaamini Kaizer Chiefs haiwezi kufikiria tena kuialika timu yetu kwa ajili ya mechi za kirafiki,” amesema.

Haji Manara ametumia nafasi hiyo kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja ili kushuhudia raha za kikosi hicho itakapomenyana na bingwa wa Ligi kuu ya Zambia na CECAFA Kagame Cup Red Arrows.

Mechi hiyo itaenda kuandika historia nyingine kwa Wananchi.

SOMA NA HII  A-Z YANGA WALIVYOIFANYIA KITU MBAYA NAMUNGO JANA....NSAJIGWA AFUNGUKA MCHEZO MZIMA...