Home Habari za Simba Leo YUSUF KAGOMA NDOTO YA UDAKTARI HADI KUCHEZA MPIRA

YUSUF KAGOMA NDOTO YA UDAKTARI HADI KUCHEZA MPIRA

habari za simba- Kagoma

YUSUF Kagoma mpenzi wa jezi namba 21, amefunguka na kueleza kuwa alikuwa na wakati mgumu katika kufanya maamuzi, ya kujiunga na Simba kwani alikuwa kishasaini na Yanga mkataba wa awali.

“Haikuwa rahisi mambo yalikuwa ni mengi lakini ukweli nilikuwa naujua mimi. Yanga sikusaini kama watu walivyokuwa wanasema bali walileta ofa kama ilivyo Simba.

“Mara baada ya Simba kunitangaza kuwa mchezaji wao kidogo nilipumua kwani hilo hata mimi nilikuwa nalisubiri kwa hamu ili kuepukana na changamoto za simu nyingi sambamba na maoni mengi ya wadau,” anasema Kagoma.

Kagoma anasisitiza kuwa alisaini upande wa Simba tu.

“Mimi ndio nilikuwa nafahamu ukweli wa mambo lakini ni kweli nilikuwa na ofa kutoka Yanga ambao ndio walikuwa wa kwanza kunifuata na Simba baadae wakaweka ofa mezani nafikiri walikuwa na uhitaji kweli kwani walifanya mambo kwa haraka,” anasema kiungo huyo.

AUCHO, KAGOMA URAIA TU

Licha ya mastaa wengi wa kigeni kutua Tanzania wakitoa changamoto kwa mastaa wa wazawa, Kagoma amesema hakuna utofauti wa ubora baina ya viungo wazawa na wageni

“Tanzania imebarikiwa kuwa na vipaji vya wachezaji wengi hasa nafasi ya kiungo hata ukifuatilia Ligi Kuu Bara unaweza kukubaliana na mimi kwani wachezaji wengi wanaofanya vizuri ni nafasi ya kiungo.

“Pamoja na timu kubwa kuwa na wachezaji wa kigeni kwenye nafasi hizo bado wanawachanganya na wazawa ambao pia wameonyesha uwezo mkubwa na wa kuvutia huku wakitajwa zaidi midomoni mwa watu,” anasema Kagoma.

Anasema utofauti upo kwasababu binadamu wanatofautiana anaweza kuwa na kitu mguuni na mwingine akakosa lakini kwa asilimia kubwa wazawa wameamka na kuonyesha kuwa wanaweza.

DAKTARI HADI SOKA

Kagoma anafichua kuwa alikuwa na ndoto za kuwa daktari lakini hazikutimia kwa sababu ya soka.

“Ndoto yangu ilikuwa ni kuwa daktari nakumbuka tangu naanza shule nikiulizwa unasoma ili uwe nani jibu lilikuwa ni kuwa Daktari ili niweze kuwatibu wagonjwa.

“Lakini soka lilichukua nafasi kubwa zaidi ya masomo pamoja na kufanikiwa kumaliza kidato cha nne lakini sikuweza kutimiza ndoto yangu na kujikuta nawekeza nguvu zaidi kwenye mpira ambao pia nilikuwa naupenda,” anasema kiungo huyo.

SOMA NA HII  AHMED ALLY ASHINDWA KUVUMILIA AITETEA SARE YA SIMBA,AFUNGUKA HAYA