Home Habari za Simba Leo SIMBA KUTESTI MITAMBO…FADLU DAVIDS AFUNGUKA UWEZO WA WACHEZAJI WAKE

SIMBA KUTESTI MITAMBO…FADLU DAVIDS AFUNGUKA UWEZO WA WACHEZAJI WAKE

Habari za Simba- Fadlu Davids

BAADA ya kujifua kwa muda wa wiki mbili sasa katika kambi iliyopo Ismailia, Misri kikosi cha Simba chini ya kocha mpya, Fadlu Davids kesho jioni kitashuka uwanjani kutesti mitambo dhidi ya El Qanah ya nchini humo.

Mechi hiyo ya kwanza ya kimataifa ya kujipima ngumu itapigwa kuanzia saa 11:30 jioni kwenye uwanjani uliopo kwenye kambi hiyo, ikiwa sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano na nafasi ya kocha Fadlu kuwasoma vyema mastaa wa timu hiyo na kurekebisha makosa mapema kabla ya kurudi nchini.

Kocha huyo alinukuliwa na mtandao wa klabu ya Simba, akijivunia kikosi alichoancho kwa jinsi kilivyo na ushindani unaompa picha ya kufanya vizuri msimu ujao, ingawa itakuwa mara ya kwanza kwake kufanya kazi Ligi Kuu Bara.

Fadlu alisema ameuona uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na alishaanza kuwapa mazoezi ya kimbinu, ufundi ili kupata timu itakayokuwa na uwezo wa kufanya vizuri wakati wa mashindano mbalimbali.

Kocha huyo aliyasema hayo, wakati anafanya mahojiano na mitandao ya kijamii ya Simba, alisema “Ushindani ni mkubwa, kila mchezaji anajituma, nimefanikiwa kuona uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, hilo ni jambo muhimu, kwani nakuwa najua jinsi ya kuwatumia.

“Ninachokifanya kwa sasa ni mazoezi ya mbinu na ufundi, ili kupata timu itakayokuwa na uwezo mkubwa wa kupata matokeo katika mashindano mbalimbali.”

Kocha huyo alisema ni kazi yake kuona kila mchezaji anafanya vizuri na kufurahia kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa.

“Ni kazi yangu kila mchezaji kushaini katika nafasi yake, ndio maana kila mmoja namuelekeza katika nafasi yake jinsi ya kutekeleza majukumu yake, pia nitaendelea kuwaona katika mechi mbalimbali ambazo tutacheza hapa zinaweza zikawa tatu,” alisema kocha msaidizi huyo wa zamani wa Raja Casablanca ya Morocco.

SOMA NA HII  YANGA YAPEWA SIKU 45 NA FIFA...YATAKIWA KULIPA DENI...ITAFUNGIWA USAJILI MISIMU MITATU