Home Habari za michezo WAZIRI CHUMI KUHUSU YANGA NA SIMBA…AWACHAMBUA WOTE

WAZIRI CHUMI KUHUSU YANGA NA SIMBA…AWACHAMBUA WOTE

habariza simba na yanga

BAADA ya mchezo wa Kariakoo Dabi kutamatika na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi ‘Gazza’ ametoa maoni yake juu ya mapungufu aliyoyaona kwa timu zote mbili.

Chumi ambaye ni mbunge wa Mafinga Mjini amesema kuwa Simba inaonekana bado haijapata muunganiko na pia kuna wachezaji hawastahili kupata nafasi ya kuanza kikosini.

Kwa upande wa Yanga, alisema kuwa kiungo wao Stephane Aziz Ki anaonekana amepungua makali na pia benchi lao la ufundi linapaswa kupunguza kulalamikia uamuzi wa refa mara kwa mara.

“Yanga wameshinda lakini kwa vyovyote kama wako makini lazima wakae chini wajipange. Naamini matarajio ya mashabiki ilikuwa wapate ushindi mnono, lakini haijawa.

“Simba bado Ina kazi ya kutengeneza muunganiko pia kuna baadhi ya wachezaji walioanza hakuna namna itabidi wakae benchi.

“Kapombe (Shomari) mbadala wake Kijili (Kelvin), Mukwala (Steven) bado sana, sijui kama Freddy (Koublan) atafaa. Balua (Edwin) mbadala wake Chasambi (Ladack).

Kibu (Denis) asubiri akili imtulie, Hussein Kazi kweli alifanya makosa ‘derby’ iliyopita lakini naona anafaa kuliko Brazamen Chamouh (Karabou) anayecheza na jukwaa,” alisema Chumi.

Kwa Yanga, Chumi alisema kuwa inaonekana Aziz Ki anakosa utulivu hivi sasa.

“Yanga, Azizi Ki anahitaji utulivu, vinginevyo suala la Hamisa Mobeto siku ya Yanga Day litamuweka katika wakati mgumu sana. Benchi la Ufundi la Yanga wajitahidi kuonesha ukomavu wa kimpira, kulalamika kila mara sio afya.

“Hongereni Yanga kwa Ushindi tunawatakia nyote (Azam na Yanga) Fainali njema,” alimalizia Chumi.

SOMA NA HII  GAMONDI AGOMA KUSHUKA KUTOKA KILELENI ATOA KAULI HII