Home Habari za Simba Leo AZIZ KI ATAJA KILICHOKWAMKISHA DILI LA KAIZER CHIEF’S

AZIZ KI ATAJA KILICHOKWAMKISHA DILI LA KAIZER CHIEF’S

Habari za Yanga leo

KIUNGO wa Yanga na MVP wa Ligi Kuu Bongo Msimu uliopita AZIZ KI amefunguka Kwa mara ya kwanza Sababu za yeye kubaki Yanga na kuzitupa ofa za timu zingine zote zilizokuwa zinamuhitaji.

“Ninajua Kaizer Chiefs na klabu zingine zinanihitaji, lakini pale mtu anapokuonesha heshima wewe pia unatakiwa kurejesha heshima” – Stephane Aziz Ki.

“Rais wa Yanga (Hersi Said ) alikuja kuniona Berkane, nilikuwa nacheza dhidi ya RS Berkane Morocco (2021), baadaye wakaja kwa familia Yangu kuongea na mimi mbele ya familia yangu. Kwangu mimii niliona ni zaidi ya heshima. Unanitaka mimi nipigie simu, sema Aziz nina ofa hii kwa ajili yako. Wao walikuja nyumbani”

“Walikuja kutoka Dar es Salaam hadi kwa familia yangu. Kwangu mimi hiyo ni too much, ni zaidi ya heshima wengine walikuwa wananipigia simu tu. Huwezi kupata watu 10 kama hao (Hersi).. Nina Appreciate sana na nina furaha na hii project na jinsi ilivyokuja.”

“Yanga walinionesha project, mpaka sasa ninaiamini project, ninamuamini Rais (Hersi). Naweza kusema Hersi Said ni kama baba yangu. Ninaiona project inavyokwenda na kazi nzuri inayofanyika, kwa sasa sio muda wa kuondoka Young Africans SC”

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA PABLO KUTIMULIWA...SIMBA WAANIKA IDADI YA MAKOCHA WALIOTUMA MAOMBI YA KAZI...