Home Habari za Yanga Leo BARUA YA WAZI KWA DENIS NKANE & SHOMARY KIBWANA…MUDA WA KUONDOKA YANGA

BARUA YA WAZI KWA DENIS NKANE & SHOMARY KIBWANA…MUDA WA KUONDOKA YANGA

HABARI ZA YANGA-NKANE

Kwenu wanangu kabisa Rafiki zangu Mimi wa nguvu, line yangu kabisa nawakubali bila Shaka ni wazima huko kwenye majukumu yenu Mimi nataka niwape ujumbe muhimu kwaajili ya vipaji vyenu vikubwa ambavyo vimewafikisha hapo Yanga SC.

Mimi chumvi ya Mawe (Mwandishi wa Habari za Michezo) ushauri wangu kwenu ni muda wa kuondoka Yanga SC umefika, mmeshafanya mambo makubwa ukiwa na Yanga mmeshashinda Kila Kikombe na Yanga ndani ya nchi hii pia michuano ya Kimataifa ya CAF.

Mmeweka rekodi ya kuvaa medali pia kuifikisha Yanga hatua robo fainali baada ya muda mrefu lakini kwasasa nafasi yenu imekuwa finyu hadhi yenu imeshuka ndani ya Yanga na thamani ikishuka hata fungu unalopata kwenye usajili wenu inawaonesha kwasasa sio watu muhimu ndani ya Kikosi cha Wananchi.

Nianze na Winga kabisa wa Mpira Rafiki yangu kipenzi Denis Daudi Nkane, unakipaji kikubwa ndiyo maana Yanga walivutiwa na wewe baada ya kuonesha kiwango Bora na Biashara United katika michuano ya Kimataifa.

Chini ya Nabi ukasajiliwa na ulikuwa unapata nafasi ya kutosha na umeweza kufunga mabao muhimu ya kuisaidia Yanga wakati huo lakini chini ya Gamondi nafasi Yako imekuwa finyu wewe fikiria katika Ligi Kuna idadi ya michezo 30 lakini dakika ulizocheza Nkane Kwa ujumla ni 40 hiyo ni hatari Kwa kipaji chako Rafiki yangu.

Kwako Kibwana Shomary katongo Mawe umefanya mambo mengi umecheza kwenye ubora mkubwa tangu utie Jangwani na kuisaidia timu kurejesha Mataji yake walipoteza Kwa misimu kama minne.

Kuna kipindi ulikuwa unapangwa namba 2 wakati mwingine unazima namba 3 ulikuwa unapata nafasi ya kutosha, ulikuwa unaitwa Kikosi cha timu ya Taifa lakini Sasa hivi ujaitwa timu ya Taifa muda Sasa na mbaya kocha Miguel Gamondi amekuwa hakupi nafasi ya kutosha.

 Na msimu huu Mpya Ameanza kukuweka jukwaani kabisa Soma alama za nyakati Kamanda wangu maana akiumia Yao Yao Beki wa pembeni anaenda kucheza Dick Job maanake thamani Yako ndani ya mipango wa kocha ni Ndogo na wewe unavyokaa nje ubora wako unapungua.

Sasa hivi unatakiwa kufanya maamuzi kwaajili ya vipaji vyenu Kwa namna ya kocha wa Yanga SC anavyopanga Kikosi chake na kufanikiwa na kupata mafanikio hakuna anayewakumbuka kwahiyo Mimi niewakumbuka ondokeni Yanga mkatafute Changamoto Mpya ninyi ni vijana

SOMA NA HII  KWA MARA YA KWANZA NABI AFUNGUKA...SABABU HIZI ZA KICHAPO CHA SIMBA