Home Habari za Simba Leo CEO FOUNTAIN GATES…KAGOMA TUMEMUUZA SIMBA…NAWASHANGAA YANGA

CEO FOUNTAIN GATES…KAGOMA TUMEMUUZA SIMBA…NAWASHANGAA YANGA

HABARI ZA SIMBA-CEO

CEO wa Fountain Gate FC (Zamani Singida Fountain Gate) amekiri kushangazwa na taarifa za Yanga kufungua kesi na kumuwekea pingamizi mchezaji Yusuf Kagoma

“Ni kweli Yanga ndio ilikua timu ya kwanza kabisa kuwasilisha Ofa ya kumuhitaji Kagoma na tuliikubali na walitanguliza Pesa kidogo

“Wakati wanafanya mazungumzo kuhusu maslahi binafsi ya mchezaji, Simba wakaingilia dili na mchezaji akaichagua Simba, Sisi kama klabu tukamuuza mchezaji alipotaka kwenda na tukawaeleza Yanga kwamba Kagoma ameichagua Simba

Yanga wakarejea tena wakataka Pesa walizotoa zihamishiwe katika uhamisho wa kiungo Aziz Andabwile na ndicho kilichofanyika na suala la Kagoma liliishia hapo

Sijui kwanini wameenda kulalamika TFF lakini kisheria Simba walifata taratibu zote na mchezaji ni mali yao halali”

SOMA NA HII  HATIMAE KRAMO ATIMKA NCHINI