Home Habari za Simba Leo KIBU DENIS APEWA PROGRAM MAALUM…KESHO 50-50 VS YANGA

KIBU DENIS APEWA PROGRAM MAALUM…KESHO 50-50 VS YANGA

Habari za Michezo

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema mshambuliaji wa timu hiyo Kibu Denis bado hajafikia katika ubora anaouhitaji, hivyo amemwandalia programu maalum ya mazoezi.

Kibu hakuwa pamoja na kambi ya Simba kwa kipindi chaote cha pre-season baada ya kutimkia Marekani kwenye mapumziko kabla ya kwenda Ulaya kwa ajili ya kujiunga na moja ya timu za Ligi Kuu ya Norway lakini dili hilo lilikufa na kurejea Simba.

“Kulingana na utimamu wa kikosi changu, nimeona nimpe Kibu mazoezi mengine tofauti ili kuwa imara zaidi na tayari kwa asilimia zote kwa sababu nina imani kubwa na mchezaji huyo anaweza akawa chachu ya ushindani kikosini hasa eneo la ushambuliaji.

“Tunahitaji kuwa na wachezaji walio tayari kiushindani kabla ya kuingia katika michuano ya ligi ya ndani na kimataifa hili nimelifanya kwa asilimia kubwa kwa wachezaji niliokuwa nao Misri,” amesema Fadlu.

Simba na Ynaga kesho zitacheza mchezo wa Nusu fainali ya kombe la Ngao ya Jamii, katika uwanja wa Mkapa majira ya saa1:00 usiku.

SOMA NA HII  WAKATI WAKIJIANDANA MECHI IJAYO...'GONJWA' JIPYA LAGUNDULIKA SIMBA...MATOLA AVUNJA UKIMYA...