Home Habari za Simba Leo KICHEKO KWA AZIZ KI…KILIO KWA NAOUMA SIMBA

KICHEKO KWA AZIZ KI…KILIO KWA NAOUMA SIMBA

habari za simba-Nouma

TAARIFA yenye machungu kwa beki mpya wa Simba, Valentin Nouma ni kwamba kocha Brama Traore, amemtema katika kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso, huku Stephanie Aziz KI wa Yanga akiendelea kupeta.

Nouma amekutana na taarifa hiyo ya kushtua ikiwa ni mara ya kwanza tangu atue Simba iliyomsajili dirisha kubwa la usajili lililopita, huku akiwa hajawahi kuanza katika kikosi hicho cha Wekundu kwenye mechi mbili za Ligi, kwani Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ aliendelea kuishikilia nafasi hiyo kwa sasa.

Wakati Nouma, aliyekuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Burkina Faso katika fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 iliyofanyika mapema mwaka huu huko Ivory Coast akitemwa, nyota wa Yanga, Azizi KI ameendelea kuaminiwa akiwa ndani ya orodha ya wachezaji 25 walioitwa kambini.

Burkina Faso inayojiandaa na mechi za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Afrika 2025, ikicheza dhidi ya Malawi na Senegal imewajumisha wachezaji watano tu wanaocheza soka Afrika.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA UBINGWA KWA SIMBA...PABLO ANYOOSHA MIKONO JUU...AWAPA RASMI YANGA UBINGWA...