Home Habari za Simba Leo KUHUSU JEAN AHOUA…HANS RAPHAEL ATAKA APEWE MUDA

KUHUSU JEAN AHOUA…HANS RAPHAEL ATAKA APEWE MUDA

Habari za Simba- Ahoua

Mchambuzi wa michezo wa Crown Media Hans Raphael amemuelezea kiungo mpya wa Simba Jean Charles Ahoua, juu ya uwezo wake uwanjani.

“Mdogo wangu Jini Charles Ahoua ana kipaji kikubwa sana,unaweza kuona vision yake akiwa na mali mguuni,ana kasi na mamlaka ya kuutumia vizuri mguu wa kulia,ila pressure ya Simba na Yanga inamtesa huyu kijana wa miaka (22).

“Ahoua hakuwahi kucheza kwenye pressure ya namna hii,Kijana ametoka Stella Club d’Adjamé,timu ambayo ilishika nafasi ya tano kwenye ligi Ivory Coast….tukumbuke hawa siyo Asec wala San Pedro.

“Ila huku amekuja kucheza Simba timu ambayo ina mashabiki 20m+ hivyo pressure ni kubwa sana.

“Jini ana kipaji kikubwa sana ila anahitaji muda wa kuzoea ligi,pia kutengeneza Chemistry na wenzake kisha mambo mengine yatafuata.” Ameandika Hans Raphael.

SOMA NA HII  HUYU HAMZA ANAIFANYA SIMBA IFAIDIKE KWA MTINDO HUU.