Home Habari za Simba Leo MANULA, ONANA, LAWI WAKOSEKANA SIMBA…CHAMA LAO LIKO HIVI

MANULA, ONANA, LAWI WAKOSEKANA SIMBA…CHAMA LAO LIKO HIVI

Habari za simba

SIMBA imetambulisha kikosi cha wa wachezaji 30 kwa ajili ya msimu 2024/25 huku majina ya Lameck Lawi na Israel Mwenda yakikosekana.

Simba walimtambulisha Lawi kama mchezaji waliyemsajili akitokea Coastal Union, lakini uongozi wa timu ya beki huyo ulikanusha na kuweka wazi kuwa bado ni mchezaji wao.

Baada ya timu hizo kung’ang’aniana, Simba ilipeleka malalamiko Kamati ya Hadhi ya wachezaji kwa ajili ya kupeleka malalamiko juu ya mchezaji huyo na kesi ilisikilizwa huku kinachosubiriwa ni uamuzi.

Lawi yupo nchini Ubelgij anaendelea kujifua na timu ya K.A.A Gent ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini humo.

Wakati Mwenda ambaye aliongezwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba pia hayupo kwenye kikosi kilichotangazwa leo.

Tunafahamu kuwa Israel Mwenda amejiunga na Singida Black Stars na ndio timu atakayoitumikia msimu ujao.

Na ilishawahi kuripotiwa kwamba sababu za beki huyo kuondoka Simba ni kutokana na waajiri wake wa zamani kushindwa kuachana na Shomari Kapombe ambaye walimuahidi Mwenda kuwa watamuacha kabla ya kumuongeza mkataba mpya.

MANULA SAHAU

Wakati huohuo aliyekuwa kipa namba moja wa timu hiyo, Aishi Manula alisahaulika kutambulishwa kikosini.

Ahmed Ally, ofisa habari wa timu hiyo ndiye aliyekuwa anataja majina ya wachezaji wa Simba msimu ujao akiwataja makipa wanne huku Manula akisahaulika na kujatwa baadaye.

Manula alikumbukwa muda mfupi baada ya kikosi cha Simba kupiga picha ya pamoja na ndipo Ahmed alipomtaja na kusema kuwa alimsahau kimakosa.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUONA MAZOEZI YA MBRAZILI...KAPOMBE AVUNJA UKIMYA SIMBA...