Home Habari za Simba Leo FADLU DAVIDS APITIA NJIA ZA JURGEN KLOPP

FADLU DAVIDS APITIA NJIA ZA JURGEN KLOPP

habari za simba-fadlu

LIVERPOOL kabla ya Jurgen Klopp alishawahi kupita kocha Bill Shankly ambaye alikuwa na mafanikio makubwa ndani ya Anfield lakini baada ya hapo Liverpool ilipitia kipindi kigumu mpaka pale ambapo Mjerumani Jurgen Klopp alikuja kuirudisha Liverpool kwenye reli yake.

Miaka zaidi ya 20+ bila kombe la ligi kuu England hapo bado walikuwa miaka zaidi ya kumi bila taji la UEFA champions league na mara nyingi hawakuweza hata kufuzu kucheza michuano ya Ulaya,Ujio wa Jurgen Klopp ulifufua matumaini makubwa kwa Liverpool na alirudisha furaha kwa wana Liverpool.

Makombe yote ambayo Liverpool alishiriki chini ya Jurgen Klopp alifanikiwa kuyashinda japo sio kwa wingi lakini alifuta vumbi kwenye makabati ya makombe pale Anfield, UEFA dhidi ya Tottenham Hotspur na ligi kwenye race dhidi ya Manchester city ya Pep Guardiola sio easy task ila Jurgen Klopp aliaminiwa na kupewa muda.

Leo hii Simba ya Tanzania imepitia depression ya miaka mitatu bila kikombe chochote cha ligi na FA imebadilisha makocha mara nyingi lakini still haijafanikiwa na sasa ipo chini ya FALDU DAVIDS kutoka South Africa ambaye ameipokea Simba kwenye nyakati ambazo inahitajika zaidi kurudi kwenye reli yake.

Kama ambavyo management ya Liverpool ilimpa muda Jurgen Klopp mpaka pale ambapo aliitengeneza Liverpool tishio duniani basi ndivyo ambavyo Simba inatakiwa kufanya kwa FALDU DAVIDS kwani kubadili makocha sio solution ya mafanikio kwenye timu.

SOMA NA HII  AL HILAL YAMCHUKUA KRAMO WA SIMBA...SABABU NI HIZI