Home Habari za Simba Leo AL HILAL YAMCHUKUA KRAMO WA SIMBA…SABABU NI HIZI

AL HILAL YAMCHUKUA KRAMO WA SIMBA…SABABU NI HIZI

Habari za Simba leo

SIMBA Wamefikia makubaliano na Mchezaji wake Aubin Kramo, kumtoa kwa mkpo kwenda kucheza Al Hilal ya Sudan, hii ni baada ya mvutano wa muda mrefu ambapo Kramo alikuwa hataki kutolewa kwa mkopo.

Kramo tangu ajiunge na Simba msimu uliopita akitokea ASEC Mimosas ya kwao Ivory Coast hakuwahi kuitumikia kwenye mechi za mashindano kutokana na kukabiliwa na majeraha ya muda mrefu, japo makocha waliofundisha kikosi hicho kwa nyakati tofauti walikiri anajua mpira.

Hata hivyo, winga huyo ilielezwa ameshapona na angebakishwa kikosini kwa msimu ujao, kabla ya mambo kubadilika kwa kuelezwa Simba imeamua kumtoa kwa mkopo Sudan, baada ya kushindwana kuachana jumla kwa sababu ya mkataba alionao na klabu hiyo.

Mmoja wa vigogo wa Simba, aliliambia amefichua kuwa, pande zote mbili zimekubaliana na sasa Kramo atakuwa sehemu ya wakali wa Sudan ambao wataicheza Ligi Kuu ya Sudan huko Mauritania baada ya kushindwa kucheza nchini kwao kutokana na hali mbaya za kiusalama zinazochangiwa na machafuko.

“Mkataba wake ulikuwa na mambo mengi, ila kwa sasa atakwenda kucheza kwa mkopo, tunamtakia kila la kheri akawe na mwanzo mzuri,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Kramo licha ya kumuondoa katika mifumo bado alikuwa ni mchezaji wa Simba na alikuwa analipwa kama kawaida lakini sasa ni rasmi kuwa tumemalizana naye kwa makubaliano ya pande zote mbili.”

Mbali na Kramo anayeondoka Msimbazi kuwapisha majembe mapya yanayoendelea kushushwa na Simba ni pamoja na Sadio Kannoute, Pa Omar Jobe, Willy Onana na Babacar Sarr ambao wanaungana na Clatous Chama aliyetua Yanga, Henock Inonga aliyejiunga na FAR Rabat ya Morocco na Luis Miquissone aliyerejea UD Songo.

SOMA NA HII  KUTOKA SUDAN: WENYEJI WA SIMBA WAMKUNG'UTA MTU GOLI 5 BILA...ZORAN NA JESHI LAKE KUANZA KAZI KESHO...