Home Habari za Simba Leo SIMBA YATUA KWA AWESU..YANGA INAMTAKA MATANIAH

SIMBA YATUA KWA AWESU..YANGA INAMTAKA MATANIAH

HABARI ZA SIMBA AWESU AWESU

Simba inadaiwa kuwa mbioni kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Awesu Awesu kutoka KMC kwa mkataba wa miaka miwili.

Mchezaji huyo anakaribia kujiunga na Simba baada ya kumaliza mkataba wake na KMC.

Awesu ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na pia winga, ingawa kuna nyakati amewahi kutumika kama kiungo wa ulinzi.

Awesu anaachana na KMC baada ya kuitumikia kwa misimu mitatu tangu 2021 aliposajiliwa akitokea Azam FC.

Kiungo huyo pia amewahi kuzichezea Mwadui FC na Madini FC.

WINGA wa kimataifa wa Madagascar, Tendry Mataniah anahusishwa kujiunga na mojawapo wa vigogo vya soka nchini, Simba na Yanga.

Nje na watani hao wa jadi, klabu ya AS Vita ni miongoni mwa timu zinazowania saini ya winga huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyekuwa akikipiga CNaPS Sport.

KIUNGO aliyekuwa akikipiga Ihefu (sasa Singida Black Stars), Duke Abuya inaelezwa yupo katika mazungumzo ya kujiunga na Coastal Union itakayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Inadaiwa Abuya aliyemaliza mkataba na Singida ni pendekezo la kocha David Ouma akitaka kuibeba timu katika michuno ya CAF kwa uzoefu alionao.

SINGIDA Black Stars, unadaiwa kuridhia kutomuongezea mkataba mpya aliyekuwa nyota wa timu hiyo, Ezekiel Mwashilindi msimu ujao.

Nyota huyo inaelezwa siyo chaguo la Kocha Patrick Aussems aliyependekeza asiongezewe mkataba mpya, huku ikielezwa huenda akaibukia chama lake la zamani la Tanzania Prisons.

SOMA NA HII  AHMED ALLY AMALIZA UTATA...AMKATAA DULLA MAKABILA