Home Habari za Simba Leo KICHUYA: LILE BAO KONA SIO BORA KWANGU

KICHUYA: LILE BAO KONA SIO BORA KWANGU

habari za simba- shiza kichuya

Kichuya ni jina kubwa kwenye anga ya michezo nchini kutokana na winga Shiza Ramadhan Kichuya ambaye kwasasa anakipiga JKT Tanzania kutambulika zaidi kwa jina hilo, lakini unaambiwa jina hilo ni la utani.

Ipo hivi;

Wengi wanafahamu kuwa Kichuya ni jina la ukoo wa mchezaji Shiza, lakini unaambiwa kuwa hilo ni jina la utani na lilitokana na baba mzazi wa mchezaji huyo kipindi hicho anacheza soka kama anavyothibitisha winga huyo.

“Nilipata historia ya jina hilo na kuamua kumuuliza baba ambaye alinijibu kuwa siyo jina la ukoo na ni watu wengi hawafahamu,” anasema.

“Jina la ukoo wetu ni Yahya, nikamuuliza baba ilikuwaje sasa Kichuya, ndipo aliponiambia kuwa kipindi anacheza soka akitumika katika nafasi ya kiungo mshambuliaji, ndio alipachikwa jina hilo.”

Shiza anasema licha ya baba yake kutokucheza soka la ushindani, lakini kwa mujibu wa masimulizi aliyopata, alikuwa bora sana zaidi yake na anabainisha kuwa

wakati yeye alivyokuwa akicheza soka wakawa wanamuita ni mtoto wa Kichuya na ndipo jina hilo likakua kwake pia.

“Hata nilipokuwa naanza shule kwenye vyeti vyangu nilikuwa naandika Shiza Ramadhan Kichuya kwasababu nilikuwa sifahamu, baadaye nilipoanza kubadili kwa kuandika Yahya, tayari jina la Kichuya lilishakua na watu wanalifahamu hilo.”

Anasema hadi sasa bado hajafahamu kwanini baba yake aliitwa Kichuya kwasababu alipomuuliza kwanini aliitwa hivyo hakumpa ufafanuzi wa chanzo.

Kichuya alitaja tukio jingine kubwa alilowahi kufanyiwa kwenye maisha yake ya mpira lililomfanya aingie kwenye nyumba ya watu bila kugonga hodi.

KUVAMIWA NA MASHABIKI

Wakati inafahamika soka ni mchezo wa burudani, unaambiwa kwa mashabiki ambao hawana uvumilivu na wanaumizwa na matokeo hilo hawaliamini kama anavyofunguka Kichuya.

“Hili tukio sitakaa nikalisahau, nikiwa Mtibwa Sugar ndiyo kwanza nimepandishwa kutoka timu ya vijana na kocha akiwa Mecky Mexume klomnal licho, nilikimbizwa

“Hili tukio sitakaa nikalisahau, nikiwa Mtibwa Sugar ndiyo kwanza nimepandishwa kutoka timu ya vijana na kocha akiwa Mecky Mexime kipindi hicho, nilikimbizwa Turiani – Manungu,” anasema.

“Nakumbuka tulitoka kucheza mechi ya ligi. Nilikuwa ndiyo kwanza nimetoka kupandishwa katika kikosi cha wakubwa, kukawa na mechi nyingine ya mtaani na viongozi wa Mtibwa Sugar walikuwa na timu yao, mchezo ulikuwa wa nusu fainali, hivyo wakaja kuchukua wachezaji wa Mtibwa Sugar na mimi nikiwamo.”

Kichuya anasema aliingia kipindi cha pili, timu ya mabosi wake ilikuwa tayari imefungwa bao moja na wapinzani wao walikuwa kina Hussein Javu, mchezo ulichezwa kwenye Uwanja wa Chamazi upo Turiani.

“Nillingia kipindi cha pili mimi na Ismail Mhesa na Jafar Kibaya, tulifanikiwa kuchomoa bao la kwanza dakika za jioni, ‘niliondoka na kijij’ nikatoa pasi mwenzangu akaunga kwa kichwa tukapata bao la pili,” anasema.

“Sina hili wala lile nikajua hakuna kitakachotokea,

“Niliingia kipindi cha pili mimi na Ismail Mhesa na Jafar Kibaya, tulifanikiwa kuchomoa bao la kwanza dakika za jioni, ‘niliondoka na kijij’ nikatoa pasi mwenzangu akaunga kwa kichwa tukapata bao la pili,” anasema.

“Sina hili wala lile nikajua hakuna kitakachotokea, nakumbuka nguo zangu nilivulia upande mwingine na mara baada ya mchezo kuisha nilikuwa ng’ambo tofauti na zilipo nguo, wahuni walipotoka sikujua kama wananifuata nikajua wanashangilia.”

Kichuya anasema alisikia sauti kutoka mbali inamwambia kimbia wanakufuata wewe hao ndipo alipoanza kukimbia akiwa na bukta na njumu mguuni na kuingia kwenye nyumba ya watu bila hodi na nyuma akifuatwa mbio.

“Kwenye kundi la watu waliokuwa wananikimbiza kulikuwa na mashabiki wa timu niliyokuwa naichezea, nikasikia ‘simama’, nikajiuliza sasa nisimame vipi wakati watu wana hasira na mimi? Hata angekuwa kaka yangu nisingefanya hivyo.

Nilipozama ndani kwa watu nilitokea mlango wa nyuma nikaruka ukuta breki ya kwanza kambini Turiani. Hilo ndiyo tukio sitakaa kwenye soka,” anasema Kichuya kuhusu mashabiki waliojawa na hasira naye baada ya kuizamisha timu yao kwa kiwango chake alichoonyesha alipoingia ‘sub’.

SIO BAO LAKE BORA

Mashabiki wa soka nchini daima watalikumbuka bao la Kichuya alilofunga katika dakika za jioni dhidi ya Yanga wakati akiitumikia Simba.

Siku hiyo katika Dabi ya Kariakoo, Yanga ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa kiutata na Hamis Tambwe ambaye alionekana akiumiliki mpira kwa mkono kabla ya kwenda kuweka bao la kuongoza.

Na wakati mashabiki wakidhani mechi ingeisha kwa ushindi wa bao hilo moja, Simba ilipata kona katika dakika 87. Kichuya akaenda kupiga kona.

Alichonga kona moja matata sana ya kiwango cha dunia. Mpira alioupiga ulikwenda moja kwa moja wavuni na kuandika historia ya aina yake huku wasanii wa Bongofleva wakimuimba katika nyimbo kama ‘Kichuya

kona’.

Licha ya bao lake hilo kutajwa kuwa ndio bao bora na wadau wa soka, Kichuya anaweka wazi kuwa kwake bao bora ambalo hatakaa alisahau, alilifunga dhidi ya Ndanda FC kabla nalasnuka derala na veve alikuwa anaitumikia Simba kipindi hicho.

“Bao langu bora nilifunga dhidi ya Ndanda, kona ilichongwa na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, alichonga mpira wa kona ambao ukatemwa na kipa Jackson Chove na kurudi nje kidogo ya 18 haukutua chini niliunganisha moja kwa moja na kutinga wavuni.

“Hilo bao linalotajwa na wengi kuwa ni bora nikiwafunga Yanga kwa kona ya moja kwa moja nillbahatisha tu, mimi sio mzuri kwenye mambo ya kuchonga kona, bao dhidi ya Ndanda nilitumia mguu wangu wa kushoto na kuachia shuti kali ambalo lilikwenda moja kwa moja wavuni,” anasema Kichuya akilitaja bao hilo kuwa hatalisahau.

BAO YANGA, BABA UBAYA NOMA

Wakati bao la Kichuya aliloifunga Yanga kwa kona akikiri kuwa lilimuingizia zaidi ya Sh40 milioni kutoka kwa wadau, mwenyewe anafunguka kuwa alibahatisha kwani hana ufundi wa kufanya hivyo akimtaja Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kuwa ndiye fundi wa hizo kazi.

“Mabao ya kona kuna mchezaji anaitwa Baba Ubaya huyo habahatishi ni fundi maeneo hayo, amefunga zaidi ya mabao manne kwenye mechi tofauti. Nafikiri huyo ndiyo anafaa kupewa sifa hizo siyo mimi,” alisema Kichuya.

SOMA NA HII  SIKU 2 KABLA YA MECHI NA ASEC MIMOSA...FREDDY 'ATINGISHA KIBUYU' SIMBA...