Home Habari za Yanga Leo YANGA WAPITIA ZENJI KUINGIA MAKUNDI YA CAF

YANGA WAPITIA ZENJI KUINGIA MAKUNDI YA CAF

Yanga SC

YANGA inayonolewa na Muargentina Miguel Gamondi, itakuwa na kazi ya kusaka ushindi utakaowafanya waingie hatua ya makundi kwa mara ya pili baada ya kukaa takribani miaka 25.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo uliopita wakiwa ugenini ubao ulisoma

CBE SA 0-1 Yanga bao la ushindi likifungwa na Prince Dube dakika ya 45 akitumia pasi ya Aziz Ki.

Mchezo ujao kimataifa kwa Yanga watakuwa Uwanja wa New Amaan

Complex dhidi ya CBE SA ambapo tayari timu imerejea Bongo kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 2:30 usiku kwa kila timu kusaka ushindi ndani ya uwanja huku Yanga wakiwa wametanguliza mguu mmoja kutinga hatua ya makundi.

Jumamosi Yanga wakimaliza kazi yao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba itakuwa kwenye Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Mkapa itakuwa dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo uliopita ugenini baada ya dakika 90 ubao ulisoma Al Ahly Tripoli 0-0 Simba hivyo mshindi kwenye mchezo wa Jumapili atafungua ukurasa wake kutinga hatua ya makundi kimataifa.

SOMA NA HII  KISA KIPIGO CHA WATUNISIA....MASHABIKI YANGA 'WAGUGUMIA NA UMBILIKOMO' WA WACHEZAJI WAO...