Home Habari za Simba Leo SALEH JEMBE AMSHAURI CAMARA…LICHA YA KUFUNGA AMSHAURI JAMBO

SALEH JEMBE AMSHAURI CAMARA…LICHA YA KUFUNGA AMSHAURI JAMBO

Karibu Tanzania Moussa Pinpin Camara, wewe si kipa bora wa kwanza kufungwa Tanzania, nikuahidi. UTAFUNGWA TENA..

Hakuna KIPA ASIYEFUNGWA lakini gumzo huwa ni amefungwaje. Mabao mawili dhidi ya Kostal Union yanakupa majibu na tafakur kuwa ligi uliyopo si lelemama…si nyepesi na inawezekana kila mechi ni kama mechi ya Confederetion Cup au Champions League.

Angalia mabingwa wa Djibouti, Somalia, Eritrea, ikiwezekana hata wa Uganda, ukiwapa nafasi hapa hawashiki 10 Bora ligi hii.

Vipaji ni vya kumwaga, ushindani ni bora mara 10 ya utokako.

Kwangu mabao uliyofungwa ni HONGERA KWA

WAPIGAJI….bao la kwanza HALINA MWENYEWE.

Bao la pili unahusika ingawa modern football inakulazimisha kufankufanya uliculichofanya lakini wenzako HAWAKUKULINDA…

ANYWAY yamepita lakini PICHA UNAYO….

KARIBU NBC PREMIER LEAGUE

SOMA NA HII  SAFARI YA KIBWANA JANGWANI KIZUNGUMKUTI...LOMALISA AUNGUZA KIBANDA...SIJUI ITAKUAJE?