Home Habari za Yanga PAMOJA NA VIPIGO MFULULIZO ….MWAMNYETO AVUNJA UKIMYA YANGA….GAMOND ATAJWA…

PAMOJA NA VIPIGO MFULULIZO ….MWAMNYETO AVUNJA UKIMYA YANGA….GAMOND ATAJWA…

Habari za Yanga leo

NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amesema hasira za kufungwa michezo mwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC na Tabora United, watazimalizia kwa Al Hilal Omdurman ya Sudan, Novemba 26, mwaka huu, itakaposhuka Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mwamnyeto, alisema kwa sasa wamesahau kila kitu, ikiwamo vipigo hivyo, lakini bado wana hasira moyoni mwao na wanataka kuitoa kwa wapinzani wao hao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Alisema mara nyingi michezo ya kimataifa inakuwa ya kiufundi zaidi na si ya kukamiana kama kwenye mechi za ligi, hivyo wanaamini kuwa hasira zao watazimalizia huko, kwani moja ya malengo ambayo wamejiwekea ni kuanza vema mechi ya kwanza ya hatua hiyo.

“Tunaendelea vizuri na mazoezi, siku ya kwanza tulianza na mazoezi ya ‘gym’, leo (juzi), tumeanza mazoezi ya uwanjani kujiandaa na mchezo wetu wa kwanza Ligi ya Mabingwa.

“Tunajua hatujafanya vema kwenye michezo yetu miwili mfululizo ya Ligi Kuu, lakini mashabiki wetu wasife moyo, tumeona makosa tumeanza kuyasahihisha mazoezini, nadhani hayatojirudia tena,” alisema beki huyo wa kati.

Alisema tayari, Kocha Mkuu, Miguel Gamondi (kabla hajafukuzwa kazi hivi leo), ameshawapa programu ya kuifanya kwa wiki nzima ili kujiweka sawa kuelekea kwenye mchezo huo.

“Hivi ninavyozungumza tunazifanyia kazi programu za mwalimu na lengo ni kushinda mchezo ili kuanza vema kwenye mchezo wa mwanzo wa hatua ya makundi, tunawasubiri na wenzetu ambao wamekwenda kwenye vikosi vya timu za taifa warudi tuungane ili tuwe kamili,” alisema.

Yanga ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Azam, Novemba 2, kabla ya Novemba 7 kupokea kipigo kingine cha mabao 3-1 dhidi ya Tabora United jambo ambalo lilizua mtafaruku kidogo ndani ya klabu hiyo mpaka kufikia hatua ya kumfuta kazi Kocha wao Mkuu Miguel Gamond pamoja na Msaidizi wake.

Naye daktari wa klabu hiyo, Mosea Matutu, alisema mchezaji Yao Kouassi, amerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa wiki mbili kutokana na homa, huku Aziz Andambwile na Shadrack Boka, wakiwa bado wanapatiwa matibabu.

“Tumekuwa na majeruhi kipindi cha nyuma, lakini kwa sasa wanarejea, Kouassi amerejea, yeye alikuwa na homa, alikuwa nje kwa wiki mbili ameanza mazoezi na mwenzake, Andambwile atarejea baada ya siku 10, Boka naye amekuwa na tatizo la kifundo cha mguu, yeye atakuwa nje kwa wiki mbili,” alisema.

SOMA NA HII  KWA KAULI HII YA AJABU YA MWAKALEBELA KUHUSU CAF...INADHIHIRA MAWAZO NA MITAZAMO YA YANGA KWA UJUMLA...