BIGIRIMANA AANZA KUITISHA SIMBA
KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga Mnyarwanda, Issa Bigirimana ‘Walcott’ amesema kuwa katika kuthibitisha ubora wa ufungaji anaanza na AS Vita wanafuatia watani wao Simba.Staa huyo aliitoa kauli hiyo, akiwa kambini mkoani Morogoro ambako wameingia tangu Jumatatu iliyopita wakijiandaa na msimu mpya wa ligi pamoja na tamasha lao la Wiki ya Mwananchi litakalofanyika Agosti 4, mwaka huu.Katika tamasha hilo, Yanga...
IGHALO SHUJAA WA NIGERIA ANAYENUKIA KUTWAA KIATU CHA UFUNGAJI BORA AFCON
ODION Ighalo mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Nigeria anatazamiwa kumaliza michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri akiwa mfungaji bora.Ighalo ni shujaa wa Nigeria kwani aliipa ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo dhidi ya Tunisia ambao ulikuwa wa kumtafuta mshindi wa tatu uliochezwa Jumatano.Mpaka sasa ametupia mabao matano, akiwaacha kwa mbali washambuliaji hatari ambao ni Sadio Mane wa Senegal,...
YANGA YAZIDI KUWA YA MOTO, YAITWANGA MORO KIDS 2-0, BALINYA ATUPIA
Mabao ya Balinya na Paul Godfrey yameiwezesha Yanga kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Moro Kids leo mjini Morogoro.Bao la Balinya limepatikana kwa njia ya penatiYanga imefanikiwa kupata ushindi huo ukiwa ni mchezo wa kirafiki uliomalizika muda mchache uliopita.Ushindi huo unakuwa wa pili mfululizo kwa Yanga baada ya mechi ya kwanza kushinda mabao 10-1 dhidi ya Tanzanite Academy.Kikosi...
JUMA KASEJA AFICHUA SIRI YA KUDUMU KWENYE UBORA WAKE
JUMA Kaseja, mlinda mlango namba moja wa kikosi cha KMC ambaye ameitwa pia kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kitakachocheza michuano ya Chan amesema kuwa siri ya kudumu kwenye ubora wake ni nidhamu.Tanzania itamenyana na Kenya Julai 28 uwanja wa Taifa na inatarajia kuingia kambini Julai 21.Akizungumza na Saleh Jembe, Kaseja amesema kuwa mchezo wa mpira una...
SIMBA NI MWENDO WA DOZI TU AFRIKA KUSINI
SIMBA hawataki utani msimu wa 2018-19, wakati Meddie Kagere, Francis Kahata, Deo Kanda na Sharaf Shiboub wakinogesha kambi leo tena dozi imeendelea kama kawaida.Simba kambini Afrika Kusini inapiga dozi ya mara mbili kwa siku asubuhi na jioni ili kujiweka fiti zaidi.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesema kuwa hesabu kubwa ni kuimarisha kikosi kiwe na ushindani kitaifa na...
AZAM FC WATAKA KUCHEZA MECHI MBILI TU KAGAME
ETIENNE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa hakuna wanachofikiria zaidi ya ubingwa.Azam FC imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuibamiza mabao 2-1 TP Mazembe kwenye mchezo wa robo fainali leo wana kazi mbele ya Manyema FC mchezo wa nusu fainali kombe la Kagame."Hakuna kingine ambacho tunakiwaza kwa sasa zaidi ya kucheza mechi mbili ambazo...
POLISI TANZANIA YABAKISHA WAWILI TU KWA SASA
SELEMAN Matola Kocha wa Polisi Tanzania amesema kuwa bado wachezaji wawili ili akamilishe kukisuka kikosi chake kipya.Matola amesema kuwa hadi sasa amesajili wachezaji 11 kati ya 13 aliokuwa anawahitaji kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara."Nahitaji kuwa na kikosi imara na kitakacholeta ushindani msimu ujao, kwa sasa zimebaki nafasi mbili tu ili kukamilisha usajili," amesema.
FAINALI YA KIBABE LEO AFCON, SENEGAL V ALGERIA
MCHEZO wa fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) kati ya Senegal na Algeria, unachezwa leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo uliopo Cairo, Misri.Awali mchezo huo ulipangwa kuchezeshwa na mwamuzi wa kati Victor Gomes raia wa Afrika Kusini, lakini yamefanyika mabadiliko na sasa atakuwa Sidi Alioum raia wa Cameroon.Senegal licha ya muda mrefu kuwa na...
TECNO YAINGIA MKATABA MPYA NA MABINGWA WA ENGLAND MACHESTER CITY
Kampuni ya simu maarufu nchini TECNO mobile imeongeza mkataba wake na klabu bingwa ya England yenye makazi yake jijini Manchester, yaani Manchester City. Mkataba huo umesainiwa nchini India huku mafanikio yakionekana katika ushindi wa mabao 4-1 kwenda fainali dhidi ya West Ham kutoka London katika mashindano ya ASIA.Ushiriakiano na klabu ya Man City unalenga kufikisha lengo la TECNO kuwaletea furaha...
MANCHESTER CITY YAMTOLEA UVIVU LEROY SANE
PEP Guardiola Meneja wa Manchester City amesema kuwa kwenye kikosi chake kama kuna mchezaji anataka kusepa ruksa yeye hana hiyana anachotaka kuona kila mchezaji awe na furaha ndani ya timu hiyo.Bayern Munich imesema kuwa inamtaka nyota wa kikosi hicho Leroy Sane na meneja huyo kasema hana hiyana asepe tu."Kama Sane anataka kuondoka hapa sio vibaya iwapo ataruhusiwa ili wengine...