WALIOKATAA FEDHA ZA UWOYA GLOBAL WAPEWA KITITA
UONGOZI wa Global Publishers umewapongeza kwa kuwapa kitita cha fedha wanahabari wake, Imelda Mtema na Hillary Daudi, kwa kuonesha weledi wa kutogombea fedha wakati mwigizaji wa Bongo Movies, Irene Uwoya alipowamwagia fedha waandishi wa habari waliojitokeza katika Ukumbi wa Hyatt Kilimanjaro jijini Dar, hivi karibuni kwenye mkutano ulioitishwa na wasanii wa tasnia ya filamu nchini.Tukio hilo la Uwoya lilielezwa...
HILI NDILO KUNDI LA TANZANIA KUFUZU AFCON CAMEROON 2021
Timu ya Taifa ya Tanzania imeanzia hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Fainali ya Mataifa ya Afrika mwaka 2021 itakayofanyika nchini Cameroon.Tanzania imepangwa kundi J ikiwa na timu zifuatavyo Tunisia, Libya na Equatorial Guinea.
NYOTA WANNE WA SIMBA WATUA AFRIKA KUSINI, WAANZA KAZI RASMI
TAYARI nyota wanne wa Simba ambao walikuwa wamekwama kukwea pipa na kujiunga na timu nchini Afrika Kusini wameshatia timu na leo wamefanya mazoezi na wachezaji wengine.Wachezaji hao ambao ni Meddie Kagere, Deo Kanda, Francis Kahata na Sharaf Shiboub walikwama kuondoka na timu Jumatatu kutokana na kushughulikia paspoti.Simba imeweka kambi ya muda wa wiki mbili nchini Afrika Kusini kwa ajili...
AZAM FC: KESHO HAO MANYEMA WANAKAA
IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kesho watapambana kuwakalisha wapinzani wao Manyema FC kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Kagame.Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa wametambua ubora na uimara wa wapinzani wao hivyo watawamaliza mapema."Wapinzani wetu wapo imara, tumewaona kwenye mchezo wao dhidi ya APR, sasa tumejipanga kupata matokeo chanya hasa ukizingatia ni hatua...
VYAMA VYA MIKOA, TFF TUWEKEENI MAZINGIRA RAFIKI KWA MCHEZO WA SOKA
Na Dominick SalambaMiaka ile ya 1990, enzi za ujana wetu kipindi cha ujana wetu wakati muziki kutoka Kongo ukitamalaki katika nchi yetu zama zile muziki huu ulikuwa unaitwa disco toto ambapo zilikuwa zikifika siku za sikukuu tulikuwa tuna ulamba nguo mpya,viatu vipya huku wengine wanatinga miwani na wengine kapelo halafu wote tunaelekea kwenye kumbi za disco ambazo zilikuwa chache...
MBIO ZA BAISKELI NDANI YA MAJIMAJI SELEBUKA NI MOTOOOO
Na Mwandishi Wetu, SongeaHuku mbio za baiskeli kwa afya katika Tamasha la Majimaji Selebuka linaloendelea mjini hapa zikitarajiwa kurindima kesho Jumamosi, joto limeanza kupanda baada ya washiriki mbalimbali kuanza kuwasili wakiwamo wale nyota waliotikisa kwenye mbio za mwaka jana.Mbio za Baiskeli katika Tamasha la Majimaji Selebuka zitakuwa za Kilomita 100 zikianzia Viwanja vya Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya...
AJIBU AKIONA CHA MOTO SAUZI
AKIWA Rustenburg, Afrika Kusini kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Ibrahim Ajibu na Francis Kahata wamekiona cha moto ni baada ya Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems kutumia saa mbili sawa na dakika 120 kuwakimbiza nyota hao.Hiyo, ikiwa ni saa chache tangu timu hiyo itue Sauzi na kuweka kambi kwenye moja ya hoteli nyota tano ya Royal Marang Hotel ya nchini huko...
YANGA YATANGAZA MECHI NNE ZA MAAJABU
YANGA imetangaza kwamba mwezi Agosti na Septemba watakuwa na mechi nne za kuonyesha ubora wao Afrika lakini hapa kambini pamenoga. Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu itaanza Agosti 9, ingawa ratiba itatoka baada ya kumalizika kwa fainali za Afcon kesho Ijumaa.Ndani ya miezi hiyo miwili, Yanga licha ya kwamba itakuwa ikicheza ligi ya ndani lakini italazimika kucheza mechi nne...
LIGT AUNGANA NA CR7 JUVENTUS, ASAINI MIAKA MITANO
Klabu ya Juventus imekamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Uholanzi Matthijs de Ligt.Beki huyo kutoka Ajax amekamilisha usajili huo kwa dau la euro, €75m.De Ligt mwenye umri wa miaka 19 amesaini mkataba wa miaka mitano Juventus mkataba ambao utaisha June 2024.