MSAFARA WA NANDY FESTIVAL WAPATA AJALI, MENEJA WAKE AFUNGUKA
Basi aina ya Coaster lililokua kwenye msafara wa kuelekea Nandy Festival Sumbawanga limepinduka Mikumi usiku wa kuamkia leo.Msafara huo ulikuwa na Wasanii Juma Nature, Whozu, Stamina,Nandy,Barnaba, Roma, Billnass, Ice Boy na Willy Paul.Maneja wa Nandy amesema Basi lililopata ajali kwenye msafara kuelekea Nandy Festival Sumbawanga lilikua limebeba Wapiga Band na Dancers na sio Wasanii, mpaka sasa Majeruhi wako Hospitalini...
KOCHA JULIO: YANGA NI TISHIO
MAKOCHA wawili maarufu na wenye heshima kwenye soka la Tanzania, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ na Juma Pondamali wamekiri kwamba Yanga mpya itakuwa tishio. Julio na Pondamali wamejenga heshima ndani ya Simba na Yanga wakiwa kama wachezaji na makocha.Julio ametamka kwamba katika Ligi ya msimu uliopita akiambiwa ni Kocha gani bora atamtaja Mwinyi Zahera wa Yanga kwani hajawahi kukosea tangu aanze...
WAWA: NINAONDOKA BONGO
BEKI kisiki wa Simba mwenye mwili uliojengeka kimazoezi Pascal Wawa amesema kuwa kwa sasa anatarajia kuondoka bongo muda wowote kuelekea nchini Ivory Coast kwa ajili ya mapumziko mafupi.Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa baada ya kutwaa ubingwa ndani ya kikosi cha Simba ni muda mwafaka kwake kusepa kwenda nyumbani kupumzika ili kujiandaa kwa msimu ujao."Nashukuru, kwa kushirikiana na...
MLINZI WA SHULE ALIYEMUUA MWANAFUNZI AHUKUMIWA KIFO
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Moshi imemhukumu kunyongwa hadi kufa mlinzi wa Shule ya Sekondari ya Scolastica, Hamis Chacha (30), baada ya kupatikana na kosa la kumuua mwanafunzi Humprey Makundi (16).Aidha, mahakama hiyo imewahukumu watuhumiwa wengine ambao ni mmiliki wa shule hiyo, Edward Shayo (65), na aliyekuwa mwalimu wa zamu, Labani Nabiswa (39) raia wa Kenya, miaka minne jela kila...
TFF, SIMBA WAJICHANGANYA KUHUSU SHOMARI KAPOMBE
KUFUATIA taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo kueleza kuhusu hali ya beki wa timu ya Simba na timu ya Taifa Stars, Shomari Kapombe kwamba amejitonesha majeraha yake Ofisa Habari wa Simba Haji Manara ameibuka na kuhoji kuhusu ukweli.Ndimbo alisema kuwa wachezaji wa Stars wameanza mazoezi ambapo watafanya mazoezi kwa muda wa wiki...
STARS KUMENOGA, DOZI MARA MBILI KWA SIKU
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Afcon itakayofanyika nchini Misri mwezi Juni.Stars kwa sasa imeweka kambi ya ndani kwa muda wa wiki moja ambapo baada ya kumaliza program ya mwalimu watakwea pipa kuelekea nchini Misri kuweka kambi mpaka siku ya mashindano.Kwa sasa Stars wanafanya mazoezi uwanja wa...
PLAYOFF NGOMA NI NZITO, SASA MECHI ZA MWISHO KUAMUA
Mechi zote za leo za Playoff zimekamilika kwa timu zoe kutoshana nguvu huku wote wakitamba kupata matokeo mchezo wa mwisho utakaochezwa Juni 8 mwaka huu.Mechi za mwisho ndizo ziakazoamua timu ambayo itapanda daraja ama kubaki kwenye ligi kati ya Mwadui ama Kagera kubaki TPL ama Geita na Pamba kupanda msimu ujao.FT: Pamba SC 0-0 Kagera Sugar, uwanja wa Nyamagana...
KWA USHINDANI ULIOPO KWA SASA KILA TIMU ISAJILI KIUFUNDI NA SIO BORA LIENDE
KATIKA vitu ambavyo viliziangusha timu nyingi zilizoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 ambao ulimalizika hivi karibuni, ni suala zima la usajili.Usajili huo ni ule wa dirisha kubwa ambao ulifanyika kabla ya kuanza kwa msimu pamoja na dirisha dogo ambapo una kawaida ya kufanyika mwishoni mwa mwaka.Timu nyingi zinapomaliza msimu, basi zimekuwa na kawaida ya kufanya usajili wa...
KESI YA AVEVA, KABURU, HANSPOPE YAKWAMA LEO
Kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Simba imeshindwa kuendelea kusikilizwa baada ya shahidi aliyeandaliwa kufiwa na kushindwa kufika mahakamani.Kesi hiyo inawakabili hao waliokuwa viongozi wa Simba Evans Aveva na Godfrey Nyange 'Kaburu' ambao wanakabiliwa na shitaka la kughushi na kutakatisha fedha huku Zachariah Hans Pope akiunganishwa katika kesi hiyo yeye kwa kudaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo za ununuzi wa nyasi...
KESI YA JAMALI MALINZI YAPIGWA KALENDA
MAHAKAMA imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya Serikali kushindwa kuleta shahidi.Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea leo Jumatatu ambapo shahidi wa 14 angetoa ushahidi wake kwenye kesi hiyo.Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliiambia mahakama kuwa hakupata muda wa kuandaa mashahidi kwa kuwa alikuwa...