DAKIKA 120 ZATIKISA YANGA

0

Kikosi cha timu ya Yanga kimewasili juzi mkoani Morogoro juzi tayari kwa kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ambapo kimejichimbia kwenye Chuo cha Bibilia maeneo ya Bigwa huku kukiwa na ulinzi mkali.Kikosi cha Yanga kipo mkoani Morogoro tayari kwa kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara katika msimu wa 2019/20 huku kikiwa kimesajili majembe mapya kadhaa.Aidha, wachezaji wote...

SHIKALO ATANGAZA SIKU YA KUTUA YANGA

0

Kipa namba mbili wa Harambe Stars na Bandari ya Kenya, Farouk Shikalo ‘Wazza’ amefichua kuwa, ilibaki kidogo tu asijiunge na Yanga, lakini sasa atatua baada ya kumalizika kwa michuano ya Kagame.Bandari hivi sasa inashiriki michuano ya Kagame ambayo inaendelea nchini Rwanda.Kipa huyo ambaye tayari amekamilisha usajili wa kutua Yanga, amesema kitendo cha Yanga kusambaza picha zake akiwa anasaini kiliwakera...

HARUNA NIYONZIMA WA SIMBA KUTIMKIA RWANDA

0

HARUNA  Niyonzima kiungo mwenye uwezo wa kuchezea mpira uwanjani namna anavyotaka inaelezwa kuwa amejiunga na klabu ya AS Kigali ya Rwanda.Niyonzima amejiunga na AS Kigali ambayo inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf) amemaliza mkataba wake na Simba hivyo anajiunga akiwa mchezaji huru.AS Kigali ni mabingwa wa FA nchini Rwanda, ataitumikia timu hiyo kwa kandarasi yake ya mwaka...

TANZIA: MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO AFARIKI

0

KWA masikitiko makubwa, uongozi wa Global Publishers, unatangaza kifo cha mwandishi wake aliyekuwa akiandikia Magazeti ya Michezo ya Championi na Spoti Xtra, Ibrahim Mressy kilichotokea mchana wa leo Julai 10, 2019 jijini Dar es Salaam.Innalillah Wainna Ilayh Rajiun!

HUYU HAPA MRITHI WA EMMANUEL AMMUNIKE

0

JOSEPH Omog, anatajwa kuwa Kocha Mkuu wa muda wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inayotarajiwa kushiriki michuano ya CHAN.Omog ambaye aliwahi kuvinoa vikosi vya Azam na Simba kwa nyakati tofauti anatajwa kurithi kwa muda mikoba ya Emmanuel Ammunike.Ammunike amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake na Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, kutokana na kuwa na mwenendo mbovu na...

TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE TANZANITE KUSHIRIKI MICHUANO YA COSAFA, VIJANA WAPATA SHAVU

0

TIMU ya Taifa ya Wanawake Tanzania 'Tanzanite' chini ya umri wa miaka 20 imepata mwaliko wa kushiriki michuano ya COSAFA ambayo inazishusisha timu za jumuia ya ukanda wa Afrika ya Kusini.Ofisa Habari wa Shirikisho la Tanzania, Clifford Ndimbo amesema kuwa michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 1 mpaka 11 mwaka huu nchi Afrika Kusini.Timu shiriki kwenye michuano hiyo...

GADIEL MICHAEL AWAANGUKIA VIONGOZI NA MASHABIKI WA YANGA

0

GADIEL Michael, bieki mpya wa Simba ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili akitokea Yanga amewaomba radhi viongozi wa Yanga na mashabiki wake.Kupitia ukurasa wa Instagram, Michael ameandika namna hii:-"Wakati mwingine mtu unalazimika kufanya maamuzi yako peke yako kwa sababu anaewajibika na maisha yako mwisho wa siku ni mtu mwenyewe. "Mpira ndio kazi yangu ya kimaisha, maamuzi niliyoyafanya yalikuwa ni muhimu...

BOVU LA MANARA KWA WACHAMBUZI KUHUSIANA NA SIMBA KUSAJILI “WAHENGA”

0

‘Hata kagere na kina Okwi wajuzi waliyasema haya haya ‘Na Haji Manara Siku hizi sijishughulishi tena na kujibu jibu makala zenye lengo la kuichafua klabu yetu,nimeacha kwa sababu moja tu,wakosoaji wetu ni wale wale na kwangu hawana jipya sababu tushawazoea na tunawajua tabia zao za kutaka wao waonekane ndio Wajuzi zaidi wa soka kuliko Watanzania wote.Lakini hili la upotoshwaji wa...

TIMU ANAYOKWENDA OKWI ILIWAHI KUNOLEWA NA DIEGO MARADONA

0

Winga Emmanuel Okwi amejiunga na timu ya Fujairah Footbal Club inayoshiriki Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu (UAE), imeelezwa.Nyota huyo Mganda anakwenda kucheza katika timu hiyo ya Ligi Kuu UAE iliyowahi kufundishwa na gwiji la soka duniani, Diego Maradona.Maradona kutoka Argentina, aliifundisha Furjairah kwa kipindi cha msimu wa 2017/18 na baada ya hapo hakuendelea.Kwa sasa kikosi hicho kinanolewa na...

BIASHARA UNITED YAFANYA BIASHARA NA AMRI SAID

0

AMRI Said amepewa kandarasi ya mwaka mmoja kuendelea kukinoa kikosi cha timu ya Biashara United ya Mara.Ofisa Habari wa Biashara United, Shomari Binda amesema kuwa unaamini uwezo na mbinu za Said ambaye ameinusuru timu kubaki kwenye ligi msimu ujao wa 2019-20."Tunaamini kwa uzoefu na mbinu alizonazo anaweza kuisaidia timu msimu ujao, kabla ya kumwaga wino tayari alishawasilisha ripoti hivyo...