RASMI HARUNA NIYONZIMA AACHANA NA SIMBA
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, amewaaga mashabiki wa timu hiyo na kuwashukuru kwa yote waliyoshirikiana kwa kipindi cha misimu miwili ndani ya klabu hiyo.Mkataba wa Niyonzima wa miaka miwili na Simba umemalizika hivi karibuni huku kukiwa hakuna dalili zozote za kuongezewa mkataba mpya na uongozi wa timu hiyo.Ikumbukwe kuwa, kiungo huyo alijiunga na Simba msimu wa 2017/18...
AJIBU PASUA KICHWA, AWAZIMIA SIMU MABOSI WA TP MAZEMBE
UNAAMBIAWA TP Mazembe, bado wamemkomalia nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu ambaye usajili wake uliingia doa kwa kushindwana kwenye malipo.Wakala wa TP Mazembe, Patrick Mazembe amesema kuwa bado Mazembe wanahitaji huduma ya mchezaji huyo ambaye msimu wa 2018/19 alikuwa ni kinara wa pasi za mwisho TPL baada ya kutoa jumla ya pasi 17."Mwanzo Ajibu alitusumbua kwa kutaka dau kubwa, kwa...
ADHABU YA WARDA WA MISRI, BADO INABAKI NA UJUMBE KWETU
Na Saleh Ally, CairoGUMZO kubwa la hapa Misri ni kuondolewa kwa kiungo Amr Warda katika timu ya soka ya taifa ya Misri.Inakuwa vigumu kujua ukubwa wa suala hilo kwa hapa Misri kama utakuwa nje au mbali na nchi hii.Kuna makundi matatu au zaidi kuhusiana na hilo, wale wanaoamini Warda anayekipiga nchini Ugiriki ameondolewa katika timu ya taifa kwa kosa...
BREAKING; SIMBA YASAJILI WABRAZIL WATATU
BEKI Tairone Santos da Silva (30) amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia timu ya Simba.Santos Amejiunga na Simba akitokea timu ya Atletico Cearense FC ya nchini Brazili.Huya anakuwa ni Mbrazili wa tatu kusaini ndani ya Simba baada ya kuanza na mshambuliaji Wilker Henrique da Silva, kiraka Gerson Fraga Viera na huyu wa leo Santos.
MATOLA WA POLISI TANZANIA KUIBOMOA YANGA NA LIPULI
BEKI wa Yanga, Haji Mwinyi, huenda akatua Polisi Tanzania iliyo chini ya Suleman Matola ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja.Mwinyi kwa sasa yupo huru kusaini na timu yoyote baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya Yanga.Pia imeelezwa kuwa Polisi Tanzania ya Matola ina mpango wa kumsajili beki wa Lipuli, Haruna Shamte ambaye ni fundi wa kupiga mipira iliyokufa ambapo ana...
DIDA NAYE MGUU NJE NDANI SIMBA, ATAJWA KUIBUKIA NAMUNGO
IMEELEZWA kuwa mlinda mlango namba mbili wa Simba, Deogratius Munish 'Dida' anaweza kusepa ndani ya kikosi hicho na kutimkia Namungo FC.Habari zimeeleza kuwa kwa sasa, Dida anamalizia mkataba wake wa mwaka mmoja ndani ya Simba hivyo kusajiliwa kwa Beno Kakolanya kunampoteza ndani ya kikosi hicho.Kakolanya amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simba akiwa ni mchezaji huru baada ya...
MAURIZIO SARRI KIBOKO KWA SIKU ANAVUTA ‘MISIGARA’ KIBAO
MENEJA wa Juventus, Maurizio Sarri amesema kuwa huwa anavuta sigara nyingi kwa siku ili kujiskia vizuri baada ya mechi.Sarri ambaye ametimka Chelsea kwa kile kilichoelezwa ktokuwa na maelewano na mashabiki kutokana na mfumo wake kwa sasa yupo Juventus."Kwa siku navuta sigara 60, ninapokuwa mchezoni huwa sijiskii kuvuta lakini lakini mda mfupi baada ya mechi ni lazima nivute," amesema Sarri.
SIMBA YAFUATA KIUNGO URENO
BAADA ya kukamilisha usajili wa Wabrazil wawili, mabosi wa Simba wamepanga kushusha kiungo kutoka nchini Ureno atakayekuja kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.Wabrazil waliowasajili Simba ni kiraka, Gerson Fraga Vieira, anayemudu kucheza beki na kiungo mkabaji na mshambuliaji, Wilker Henrique da Silva wote waliosaini miaka miwili.Simba, pia imefanikisha usajili wa kiungo mkabaji,...
MONDI AMPA MSALA KIBA!
DAR ES SALAAM: Weka pembeni nyimbo zake za mwaka huu za Tetema, The One na Inama, sasa ni zamu ya Kanyaga kutoka kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambao umesababisha kizazaa kwa hasimu wake kimuziki, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, Amani linafunguka. Mapema wiki hii, Diamond au Mondi aliachia wimbo huo ambao hadi juzi Jumanne mchana ulikuwa...
MASTAA YANGA WAANZA KUTUA AIRPORT
WACHEZAJI wapya wa Yanga na wale wa zamani wanatarajia kuanza kuingia nchini wiki hii kwa ajili ya kujiandaa na kambi ya timu hiyo inayotarajiwa kuanza rasmi Julai 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam.Tayari Yanga imeshasajili nyota 10 wapya wakiwemo wazawa ambao ni Mapinduzi Balama, Abdulaziz Makame,Ally Ally, kwa upande wa wageni ni Patrick Sibomana, Sadney Urikhob, Issa Bigirimana...