MTU KABEBA MILIONI SABA ZA SPORTPESA KWA ULAINIIIIIIII…..
Mkazi wa Kinondoni Bwana Bakari Mustapha Salum, akikabidihiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 7 mara baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 11 kati ya 13 za JackPot ya SportPesa.Kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa Bi. Sabrina Msuya.
EXCLUSIVE!! YANGA YAMALIZANA NA ALLY ALLY, AMWAGA WINO WA MIAKA MIWILI
Beki kiraka wa timu ya KMC, Ally Ally 'Mwarabu' amemalizana na uongozi wa Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwiliAlly amekuwa bora ndani ya KMC hali iliyomvutia Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera na kuacha maagizo kwamba naye aongezwe kwa wachezaji wa ndani.Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa mipango ya usajili inaendelea kwa sasa kwa wachezaji wa ndani...
MIDO WA SINGIDA KUBEBA MIL 20 YANGA
IMEFAHAMIKA kwamba mido mpya wa Yanga, Kenny Ally ambaye anaichezea Singida United atalamba milioni 20 ikiwa ni sehemu yake ya usajili.Yanga watampata mido huyo wa Singida kilaini kabisa kutokana na usajili wake kukamilishwa kila kitu na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.Taarifa kutoka ndani ya Yanga ambazo Championi Jumatatu, limezipata ni kuwa kiungo huyo atasaini kwa kiasi hicho ambacho...
KIGOGO AFUNGUKIA USAJILI WA NIYONZIMA YANGA
UONGOZI wa Yanga umekanusha tetesi za kiungo wao wa zamani Mnyarwanda, Haruna Niyonzima kuwa anaweza kujiunga tena na timu hiyo.Taarifa hizo zilianza kuzagaa juzi mitandaoni wakati tamasha lao kubwa la ‘Kubwa Kuliko’ likiwa linaendelea kwenye Ukumbi wa Dimaond Jubilee, Upanga jijini Dar es Salaam.Niyonzima ni kati ya wachezaji waliomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara...
VIDEO: ALIYEUA MWANAFUNZI WA KIU AKAMATWA NA POLISI
JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata Ernest Joseph (19) kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Anifa Mgaya, aliyefariki dunia Juni 17 baada ya kuchomwa kisu.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Jumatano Juni 19, Kamanda wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema...
SIMBA YATOA TAMKO JUU YA RAMADHANI SINGANO ‘MESSI’
UONGOZI wa Simba umesema kuwa bado una imani na mchezaji wao wa zamani, Ramadhani Singano 'Messi' ambaye ametemwa ndani ya kikosi cha Azam FC kilicho chini ya Etiene Ndayiragije.Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa ni wakati sahihi kwa Messi kutulia kabla ya kufanya maamuzi."Bado ni mchezaji mwenye akili nyingi, uwezo wake hasa wa kutumia mguu wa kushoto...
ORODHA YA NCHI AMBAZO ZIMEANDAA MARA NYINGI MICHUANO YA AFCON
MISRI ambao ni wenyeji wa michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza kufanyia Juni 21 wanashikilia rekodi ya kuandaa michuano hiyo mara nyingi Zaidi wakiwa wameandaa mara tano.Tanzania inashiriki mara ya pili ikiwa ni baada ya kupita miaka 39 mchezo wa mwisho ilishinda mbele ya Uganda kwa jumla ya mabao 3-0 uwanja wa Taifa, orodha ya nchi nyingine ni pamoja na:-Ghana imeandaa...
HUYU NDIYE RYAN MOON ANAYETAJWA KUTUA SIMBA
RYAN Moon amezaliwa September 15, 1996 Pietermartzburg-KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.Kwenye maisha ya soka yeye anacheza nafasi ya ushambuliaji na anapenda kuvaa jezi namba 7, amecheza jumla ya mechi 25 kwa mwaka 2016-17 akiwa na timu mbili tofauti ambazo ni pamoja na Martzburg United ambapo alicheza jumla ya mechi mbili na zote hizo hakufunga bao.Pia kwenye klabu yake ya Kaizer Chief amecheza jumla ya...
UNITED YAMKOMALIA POGBA
MANCHESTER United wamemkomalia kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Paul Pogba licha ya yeye mwenyewe kutaka kusepa kikosini hapo.Pogba amesema kuwa kwa sasa anahitaji kupata changamoto mpya nje ya Premier League baada ya kucheza ndani ya Manchester United kwa muda wa miaka mitatu.United wamesema kuwa watamuongezea posho na mshahara mchezaji huyo ili kupata huduma yake.
MWANTIKA AREJESHWA TAIFA STARS
Beki mkongwe nchini David Mwantika amerudishwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichopo Misri kujiandaa na mashindano ya AFCON.Mwantika amerejeshwa baada ya kuumia kwa Aggrey Morris wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Misri.Mwantika aliachwa katika mchujo wa mwisho nchini Misri uliofanyika kabla ya kuanza kwa mechi za kirafiki.Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 21 nchini humo ambapo Stars itakuwa inashiriki...