BREAKING NEWS:…BARBARA AJIUZULU SIMBA…AWAACHIA MSALA HUU WAJUMBE WA BODI…
Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, mwanamama Barbara Gonzalez ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake ndani ya klabu hiyo. Barbara ameandika barua ya kujiuzulu akibainisha sababu kuu mbili, ambapo amedai anatoa nafasi kwa Bodi mpya ya Wakurugenzi kuchagua Mtendaji Mkuu mpya atakwenda sambamba na malengo yao, pili anajipa muda wa kutimiza ndoto nyingine. Soma kwa kirefu barua ya Barbara hapa chini;
BAADA YA KUSIKIA NAMUNGO WANAMTAKA…SIMBA WAMPANDISHA DARAJA MATOLA…
Mabosi wa Simba wajanja sana, kwani baada ya kusikia kocha msaidizi aliyekuwa masomoni, Seleman Matola anatakiwa na klabu moja ya Ligi Kuu Bara, fasta wakaamua kufanya mambo kwa kumpandisha cheo ili aendelee kusalia klabuni, huku mwenyewe akifunguka kila kitu juu ya ishu hiyo. Matola amerejea hivi karibuni kutoka kwenye kozi ya ukocha wa Leseni A ya Shirikisho la Soka Afrika...
SIKU KADHAA BAADA YA KUTEMANA NA GEITA…MPOLE AVUNJA UKIMYA..AFUNGUKA MENGI YA NYUMA YA PAZIA…
Siku chache baada ya kuvunja mkataba na Klabu ya Geita Gold, kinara wa mabao wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, George Mpole amefichua kilichomfanya afikie uamuzi wa kuondoka kwenye timu hiyo, aliyoifungia mabao mawili hadi sasa katika ligi ya msimu huu. Akizungumza Mpole aliyefunga mabao 17 msimu uliopita na kumpiku Fiston Mayele wa Yanga aliyemaliza na mabao 16, alisema amefikia...
KAZE : HII YANGA KAMA SIO AUCHO NA FEI TOTO HALI INGEKUWA SIO…
Yanga imerejea jijini Dar es Salaam kutoka Lindi ilipokwenda kucheza mechi ya kufungia duru la kwanza la Ligi Kuu dhidi ya Namungo, huku kocha msaidizi wa timu hiyo, Cedric Kaze akifichua kilichowabeba kushinda kwa mara ya kwanza ugenini dhidi ya Wauaji wa Kusini na kuwataja viungo, Khalid Aucho na Feisal Salum ‘Fei Toto’. Yanga ilishinda mabao 2-0, yaliyowekwa kimiani na...
PAMOJA YA KUPITIA MAMBO MAZITO MSIMBAZI…OKWA APATA WA KUMTETEA KIBABE…
Nelson Okwa, nyota aliyesaliwa Simba kutoka Nigeria na kushindwa kukuna nyoyo za mashabiki wa timu hiyo, amepata mtetezi baada ya kipa wa Rivers United, Victor Sochima kumkingia kifua kwa kuwataka viongozi na benchi la ufundi kumpa muda ili waupate utamu wa mshambuliaji huyo. Sochima mwenye umri wa miaka 23, aliyecheza kikosi kimoja na Okwa walipokuwa wote Rivers Utd ya kwao...
WAKATI AKIONEKANA YUPO KAMA HAYUPO…SINGIDA BIG STARS KUMUOKOA AJIB…
Siku chache tangu kupata ruksa ya kufanya usajili baada ya awali kufungiwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF), mabosi wa Singida Big Stars wameingia sokoni kwa kishindo na sasa wapo hatua ya mwisho kunasa saini za mashine mbili kutokea kwenye timu mbili tofauti, akiwamo Ibrahim Ajibu. Ajibu, aliyewahi kung’ara na Simba na Yanga kwa misimu tofauti, kwa sasa anakipiga Azam...
WAKATI MAMBO YAKIZIDI KURINDIMA QATAR… HIVI NDIVYO TANAPA WANAVYOENDELEA KUIPAISHA TZ
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na taasisi nyingine za wizara ya Maliasili na Utalii (TTB, TFS) na kituo cha uwekezaji Tanzania -TIC limefanikiwa kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji zilizopo nchini katika sekta mbalimbali. Wageni kutoka mataifa mbalimbali waliofika nchini Qatar kwa ajili ya mashindano ya kombe la Dunia, wameweza kupata taarifa muhimu kwa karibu...
BAADA YA KUTUPWA NNJE KOMBE LA DUNIA…KOCHA WA BRAZIL KAONA ISIWE KESI…KAWASUSI TIMU YAO HUKO…
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Adenor Leonardo Bacchi maarufu kwa jina la Tite rasmi ameachia ngazi kukinoa Kikosi cha timu hiyo baada ya kutupwa nje ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 katika hatua ya Robo Fainali dhidi ya Croatia. Kocha Tite amechukua maamuzi hayo baada ya kutupwa nje ya Michuano hiyo mikubwa duniani inayoendelea nchini Qatar,...
TAKWIMU…MZUNGUKO UJAO TARAJIA MAGOLI ZAIDI…HISTORIA ITAANDIKWA BONGO…
Kuna ongezeko la asilimia 14 ya mabao yaliofungwa katika mzunguko wa kwanza msimu huu, timu zikiwa zimefunga 260, ukitofautisha na msimu uliopita ambapo ngwe kama hiyo yalipachikwa 228, jambo linalotoa taswira ya kupatikana mengi zaidi. Jumla ya mabao yote ya msimu wa 2021/22 yalikuwa 471, huku tayari msimu huu yakiwa yamefikiwa nusu yake, hilo linathibitisha namna msimu huu unavyoweza ukawa...
KUHUSU DILI LA KUMSAJILI FEI TOTO…AZAM FC WAANZA KUSHIKANA MASHATI…CEO AMKATAA HADHARANI…
Uongozi wa Azam FC umeshangazwa na taarifa za kuendelea kuhusishwa na Mpango wa kumsajili Kiungo wa Young Africans Feisal Salum ‘Fei toto’. Azam FC imekuwa ikihusishwa na usajili wa kiungo huyo kutoka Zanzibar kwa majuma kadhaa, huku ikielezwa tayari imeshatenga fungu maalum kwa ajili ya kuvunja mkataba wake Young Africans. Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC Abdul-Karim Amin ‘Popat’ amesema hakuna...