BAADA YA KISINDA KURUHUSIWA ….MAMBO YABADILIKA YANGA…NABI AIBUKA NA MSIMAMO HUU …
Siku moja baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitisha jina la winga wa Yanga, Tuisila Kisinda kocha Nasreddine Nabi amesema anatarajia mambo mazuri kutoka kwake.TFF, wametoa taarifa hiyo jana usiku ikieleza kuwa wamepitisha jina la Kisinda kwenye usajili baada ya Yanga kumuhamisha, straika Lazarous Kambole na nafasi yake kuchukuliwa na Kisinda ili kutimiza idadi ya wachezaji 12.Nabi amesema...
PAMOJA NA KUFANYA VIZURI….SIMBA HAWANA IMANI NA MGUNDA…KUMBE MPAKA SASA ‘ANAPIGA DEIWAKA”…
Mpaka mechi ya juzi jioni baina ya Simba na Prisons inaanza hakukuwa na kocha mzawa aliyekuwa ameomba kuifundisha klabu hiyo.Simba iko kwenye harakati za kutafuta kocha mkuu atakayerithi mikoba ya Zoran Maki aliyeachana nayo siku kadhaa zilizopita.Simba imempa kazi ya muda mzawa Juma Mgunda kukaimu nafasi hiyo, ambaye aliiongoza kushinda mabao 2-0 kwenye mechi ya kwanza ya Ligi ya...
KISA KISINDA…NABI ATANGAZA MAANGAMIZI YANGA……MGUNDA AJIKUNA KIDEVU NA MASTAA WAKE SIMBA…
Pitia Ukurasa wa mbele wa gazeti la MwanaSpoti la leo Jumamosi.
MWAMBA HUYU HAPAA…NABI ACHEKELEA KOONI KISINDA KURUHUSIWA…BOSI SIMBA AIONYA YANGA KWA WASUDANI…
Pitia ukurasa wa mbele wa gazeti la Championi la leo Jumamosi.
ISHU YA AUCHO YASHUSHA PRESHA YANGA…SASA NI UHAKIKA ASILIMIA ZOTE JAMBO LIPO….
Kiungo wa kimataifa wa Yanga, Khalidi Aucho raia wa Uganda aliyepata majeraha juzi dhidi ya Mtibwa Sugar, anaendelea vizuri kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo, Shecky Mngazija ambaye amesema anaweza kutumika hata wikiendi ijayo.“Aucho amepata majeraha ya kawaida tu kwenye mchezo huo mguu ulishtuka tukaona tusiendelee kumuacha uwanjani kwasababu angeweza kupata majeraha makubwa zaidi, ndipo mwalimu akaona ambadilishe...
BAADA YA KUPITIA MAGUMU….RONALDO AWEKA REKODI MPYA ULAYA…APIGA GOLI LA 700 MAN UTD WAKIOSHA NYOTA ….
Nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo, amefuta ukame wa mabao ndani ya miaka 16 aliyokipiga baaa ya kufunga bao kwa mkwaju wa penalti dhidi ya Sheriff Tiraspol, kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Europa uliyochezwa jana Alhamisi.Ronaldo amefunga bao hilo kwa mara ya kwanza kwenye mashindano hayo na kuweka historia maisha ya soka lake kwani hakuwahi kucheza michuano...
FEI TOTO CHANZO CHA BANGALA KUCHEZESHWA BEKI…NABI AFUNGA KESI KWA KUMKABIDHI RASMI MAJUKUMU MAPYA…
Mashabiki wa Yanga wamezoea kuona beki wao wa kati Mkongomani Yannick Bangala akicheza kiungo mkabaji lakini kocha wao Nasreddine Nabi amewaambia watulie vinginevyo pale kwa kina Feitoto hapatakalika.Nabi amesema kuwa ameona mijadala ya mashabiki juu ya kutaka Bangala arudishwe kucheza kama kiungo na kwamba amekuwa na maoni tofauti.Kocha huyo mwenye misimamo aliongeza kuwa hatua ya kumrudisha Bangala kucheza nafasi...
MERIDIANBET WAUNGA MKONO KAMPENI YA BUKU YA HEDHI SALAMA….
Meridianbet wameunga mkono jitihada za kampeni ya Buku ya Hedhi salama inayoratibiwa na Shufaa Hemed Nasoro. Kampeni hii ilikuwa imelenga kuchangisha michango ya kiwango cha angalau shilingi elfu moja kuwasaidia mabinti ambao wanapata changamoto za kumudu gharama za taulo za kike. Meridianbet, ambao ni wadau wakubwa wa shughuli za kijamii, wanaona umuhimu wa hedhi salama kwa mabinti,...
KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO….UNAAMBIWA NABI HUKO YANGA HATAKI MZAHA…APANIA KUUA ‘SISIMIZI KWA RUNGU’….
Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Nesreddine Nabi, amewahimiza wachezaji wake kuwa tayari kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Mabingwa wa Sudan Kusini Zalan FC kesho Jumamosi (Septemba 17).Young Africans itakua nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku ikiwa na mtaji mkubwa wa mabao 4-0 waliouvuna katika mchezo wa Mkondo...
SAA CHACHE KABLA YA KUKUTANA NA YANGA KESHO….WASUDAN WAENDELEA KUWEWESEKA NA MAYELE…FEI TOTO KUTIWA PINGU…
Kocha Mkuu wa Zalan, Mawein Deng amewataja Fiston Mayele na Feisal Salam ‘Feitoto’ kuwa ndio wachezaji anaowahofia zaidi hapo kesho.Wawili hao ndio walio wafunga kwenye ushindi wa mabao 4-0 huku Mayele akiingia kambani mara 3 na Fei Toto akifunga bao moja.Akizungumzia mchezo kwa ujumla alisema timu yake imefanyia kazi makosa waliyoyafanya kwenye mchezo uliopita wamejiandaa vizuri kwa mchezo wa...