Thursday, January 8, 2026
Home Blog Page 2950

ZAHERA AMZUNGUMZIA KIVINGINE KABISA SAID NDEMLA, AIBUA KIOJA KWA MKAPA

0


TIMU ya Azam FC jana Jumanne, Mei 28, 2019 wamelipa kisasi baada ya kuifunga Yanga kwa mabao 2-0, mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania bara uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bao la kwanza limefungwa na Daniel Amouh dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza na bao la pili limefungwa na Mudathir Yahya dakika ya 50.

Timu zote mbili zilikuwa zinatafuta heshima kwenye uwanja wa Taifa leo ikiwa ni mchezo wa mwisho kwa msimu huu baada ya Yanga kuifunga Azam bao 1-0 katika mchezo wa kwanza.

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema; “Said Ndemla hayupo kwenye makaratasi yangu sina habari zake.”

“…….Hii t.Shirt na kofia zimekuwa ni utambulisho wangu msimu huu bahati mbaya hatujapata ubingwa,msimu ujao ntakuja na muonekano mwengine,“

RASMI SIMBA KUWEKA KAMBI MAREKANI

0


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji na mwekezaji wa timu hiyo, mfanyabiashara Mohammed Dewji wamekubaliana kwa pamoja kuipeleka timu hiyo nchini Marekani katika kambi ya maandalizi ya msimu ujao.

Aussems amekubaliana hivyo na Mo baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Na amefunguka hivyo katika mahojiano yake Jumatatu kwenye Hoteli ya Sea Scape jijini Dar jana.

Ikumbukwe kuwa huu ni msimu wa pili kwa timu hiyo kwenda kuweka kambi nje ya nchi baada ya mwanzoni mwa msimu huu kwenda Uturuki katika kambi ambayo imewapatia mafanikio makubwa.

Aussems alisema kuwa tayari wameshakubaliana na Mo kuwa kambi ya maandalizi ya msimu ujao itafanyika katika nchi ya Marekani inayoongozwa na Rais Donald Trump.

“Maaandalizi ya msimu ujao tutaanza baada ya kukamilisha ligi ambayo Jumanne (kesho) ndiyo itakuwa inafikia mwisho baada ya kupewa kombe letu, kwa sababu tuna mengi ya kufanya ikiwemo suala la maandalizi ya kambi ya maandalizi kwa msimu ujao.

“Lakini tumeshakubaliana na jana nilikuwa na Mo mwenyewe kuongelea suala hilo wapi tutaweka kambi japokuwa uongozi wao walitaka zaidi twende tukaweke kambi nchini Ureno lakini nimemueleza Mo kwamba ni vyema tukaenda kuweka kambi nchini Marekani, jambo ambalo ameshalipitisha, hivyo kwangu nasubiria wakati uweze kufika,” alisema Aussems.

UFAFANUZI NAMNA KAGERA ILIVYOSHUKA DARAJA

0


Kwa mujibu wa takwimu kutoka Bodi ya Ligi kabla ya michezo GD ya Stand United ilikuwa -9 na GD ya Kagera Sugar ilikuwa -11 matokeo ya Leo

FT’ JKT Tanzania 2-0 Stand United 
FT’ Mbao FC 1-1 Kagera Sugar

Maana yake Stand United imebaki na pointi zake 44 na GD ya -11 na Kagera Sugar imekuwa na Pointi 44 na GD ya -11

Kwa maana hiyo GD zinafanana wote -11 kinachofuata ni Head to Head mechi ya kwanza ya Stand na Kagera ilifanyika Shinyanga na Matokeo yalikuwa 1-1 na mechi ya pili ilifanyika Kagera matokeo Stand ilishinda kwa magoli 3-1

Maana yake Stand anakuwa na Faida kwenye Head to Head. Na kwa mjibu wa takwimu hizo African Lyon na Kagera Sugar wameshuka moja kwa moja na Stand United na Mwadui FC zinacheza Play Off.

ZIDANE ANA MAMBO MANNE YA KUWEKA SAWA REAL

0


BAADA ya kufanya vibaya msimu huu wa 2018/19, uongozi wa Real Madrid unakabiliwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri msimu ujao.

Real Madrid imekamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa La Liga ikiwa na pointi 19 nyuma ya wapinzani wao wa jadi, Barcelona, ambao wamenyakua ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.

Kibaya zaidi ilitolewa kwenye hatua ya mtoano wa 16 bora na Ajax Amsterdam. Real Madrid ina rekodi mbovu katika La Liga katika misimu ya karibuni ikiwa imetwaa ubingwa mara moja wa La Liga katika misimu saba.

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ana kibarua cha kufanya mambo manne ili kuweza kurudisha makali ya timu hiyo, ambayo inashikilia rekodi ya kutwaa mara nyingi zaidi ubingwa wa La Liga na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

AMTUMIE ZAIDI VINICIUS

Vinicius Jr bado ana umri wa miaka 18 lakini katika mechi ambazo amechezeshwa ameonyesha kuwa ni moto. Atakuwa silaha ya maana ya kuongeza makali ya Real Madrid kutokana na mabeki wengi kushindwa kwenda na kasi na chenga zake. Zidane anapaswa kumsaidia Vinicius aweze kufunga mabao mengi zaidi kutokana na ukweli kuwa rekodi yake ya kufunga mabao bado sio nzuri. Tangu ameanza kujumuishwa kikosi cha wakubwa cha Real Madrid msimu wa 2018/19, amecheza mechi 31 na kupachika mabao manne.

KASI NDOGO YA MASHAMBULIZI REAL

Real Madrid inakabiliwa na tatizo la kushindwa kushambulia kwa kasi timu pinzani. Tatizo hili limejitokeza katika nyakati tofauti wakati timu ikinolewa na Julen Lopetegui, Santiago Solari na sasa Zidane. Nyota wa kutengeneza mashambulizi wa Real Madrid kama Marcelo, Toni Kroos na Isco kwa sasa wanaonekana kupungua uwezo.

Kuna mechi nyingi tu ambazo Real Madrid ilishindwa kasi na timu pinzani kama ilivyotokea kwenye mechi kadhaa msimu huu kwa mfano dhidi ya Ajax, Eibar, Huesca, Sevilla, Athletic Bilbao, Rayo Vallecano na nyingine nyingi. Zidane atapaswa kuja na maarifa mapya ya namna ya kutengeneza mashambulizi ya Real Madrid ukizingatia timu hii haina tena Cristiano Ronaldo, ambaye alikuwa tishIo kwa timu pinzani.

TATIZO LA MARCELO

Beki wa kushoto, Marcelo alikuwa anahusika kwa kiasi kikubwa kutengeneza mashambulizi ya Real Madrid. Msimu huu mara kadhaa Marcelo amekuwa anawekwa benchi na nafasi yake kuchukuliwa na kinda Sergio Reguilon. Marcelo alikuwa ni mzuri wa krosi na pasi za mabao lakini inaonekana wazi kuwa makali yake yameanza kupungua. Hata hivyo, Zidane amesisitiza kuwa ataendelea kumtumia Marcelo na beki wake wa kushoto.

MUSTAKABALI WA YOSSO

Zidane atakuwa na mtihani wa kukuna kichwa wa namna ya kuwatumia yosso kama Vincius Jr, Reguilon na Marcos Llorente. Wachezaji hawa katika nafasi chache walizopewa msimu huu walionyesha uwezo mkubwa. Vinicius alikuwa moto katika kutengeneza mashambulizi huku Reguilon akifanya kazi ya kuziba pengo la Marcelo alipopewa nafasi kama beki wa kushoto. Llorente naye amekuwa anafanya vizuri pale alipokuwa anapewa nafasi kwenye sehemu ya kiungo.

WAZAWA JIPIMENI KWENYE SURA YA JOHN BOCCO

0


Na Saleh Ally

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara kwa misimu miwili mfululizo sasa, Simba tayari wanakwenda kwenye usajili ambao utawalazimisha kuangalia kilicho sahihi zaidi.

Wakati Simba wakiangalia kilicho sahihi lazima watakuwa wanapanda kutoka hatua moja kwenda nyingine kwa maana ya ubora zaidi katika msimu ujao.

Kwa nini Simba wanahitaji kawa bora zaidi? Jibu ni kwa kuwa wameona makosa yao mengi sana wakati wakiwa katika Ligi Kuu Bara ambayo mwisho wameibuka kuwa mabingwa. Lakini wameona makosa mengi sana wakati wakishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ligi ya Mabingwa Afrika walifika katika hatua ambayo kwa muongo mzima au miaka ya hivi karibuni hawakuwa wamefikia katika hatua hiyo. Safari hii wamefikia hatua ya robo fainali ambayo ina ugumu wa juu ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Baada ya kufika katika hatua hiyo watakuwa wamejifunza mengi sana na hasa hatua ya makundi ambayo tuliona, Simba ilionekana dhaifu kiasi cha kufungwa mabao 12 katika mechi tatu tu.

Kama wastani maana yake walifungwa mabao manne kila mchezo bila ya wao kufunga hata moja lakini uhalisia unaonyesha walifungwa 5-0 mara mbili na mwisho 2-0. Hivyo wanajua wanahitaji kipi hasa.

Bila ubishi Simba wanahitaji wachezaji bora kabisa wenye kiwango kilicho sahihi ambacho kitawafikisha mbali zaidi na kuwafanya kuwa na timu imara hata ikitoka nje ya Tanzania badala ya kuwa na kikosi chenye ubora wa juu kinapokuwa nyumbani peke yake.

Ukiangalia sababu kuu iliyowang’oa ni kutokuwa imara nje ya nyumbani kwani baada ya TP Mazembe kufanikiwa kuizuia Simba nyumbani na kuilazimisha sare, basi wakawa wamemaliza kila kitu kwa kuwa wakati Simba inaondoka kwenda Lumbumbashi, hakuna aliyekuwa na matumaini ya ushindi kule DR Congo.

Kwa nini hakuna matumani? Jibu Simba haikuwahi kushinda ugenini katika kiwango hicho, badala yake hatua ya awali iliposhinda dhidi ya Mbabane Swallows. Sasa Simba inahitaji kuwa ina uwezo wa kushinda nyumbani katika kiwango cha juu zaidi ya hicho ilichokuwa nacho lakini inahitaji kushinda ugenini angalau uwezo wa uhakika wa saizi ya kati.

Haya yatawezekana kama Simba itakuwa na kikosi imara. Kikosi hicho lazima kiundwe na wachezaji bora, makocha bora kwa maana ya yule wa makipa, wa viungo, kocha msaidizi na bosi wa benchi lenyewe. Tayari wanao lakini kikubwa ni suala la kupima.

Wakati tunakwenda huko, huu ndiyo wakati mzuri wa kujitathmini kwa wachezaji wa hapa nyumbani Tanzania. Kama wachezaji wazalendo, nani anajiona yu sahihi kuweza kugombea namba au kupata nafasi Simba ambayo inafikiria ukubwa au nguvu zaidi?

Kawaida timu iliyokuwa na mafanikio zaidi na hasa kama imehusisha Bara, inaweza kuwa kipimo cha wachezaji wa nchi husika. Kwamba wanapata nafasi kiasi gani na waliopo nje ya kikosi hicho wanaweza kushindana na walio ndani ili kuiimarisha Simba.

Kiwango cha kuwaza cha Simba, kitakuwa ni nje ya Tanzania. Ukitengeneza timu bora inayoweza kushindana kiwango cha Bara la Afrika, bila shaka itakuwa na uwezo wa kushiriki vizuri ligi ya ndani.

Wachezaji wazawa hawa walio Simba hawakuwa na nafasi kubwa sana kama wageni. Angalia, mchezaji pekee ukiachana na kipa Aishi Manula unaweza kusema alikuwa vizuri sana ni John Raphael Bocco.

Nahodha huyo wa Simba ni mfano wa kuigwa na ubora wake umekuwa mchango katika kuendesha timu, kuzalisha mabao na ikiwezekana yeye mwenyewe kufunga. Achana na hivyo, angalia uchezaji wake wa juhudi, maarifa na mfano ambao hata ukimuuliza mchezaji yeyote mgeni lazima amtaje Bocco.

Bocco amekuwa mshindani wa namna, mshindani uwanjani na kiongozi sahihi. Wachezaji wengine wa Kitanzania hili limewashinda na viwango vyao vilikuwa ni vile vya kupanda na kushuka na wakati mwingine kunaweza kuwa na kisingizio cha wageni lakini kama kiwango chako ni bora, hakuna wa kukuzuia kama ambavyo Bocco ameonyesha.

Walio ndani ya Simba wanalijua hilo lakini hata walio nje bila ya ubishi watakuwa wameliona hilo na liko wazi. Nani anatamani kuwa kama Bocco au madai ya wachezaji kama Erasto Nyoni au Mohammed Hussein Zimbwe ambaye baada ya kurejesha kiwango chake kikaendelea kupanda siku hadi siku?

Kwa kipindi hiki Simba inasaka wachezaji wa kuifanya iwe bora zaidi, basi kikubwa walitakiwa jicho lao liwe Tanzania zaidi. Lakini ninaamini bado watalazimika kuwaacha wageni na kuongeza wageni tena kwa kuwa Watanzania walikuwepo lakini bado hawakuwa na ushindani bora zaidi au ubora unaoendelea.

Kuna jambo la kujifunza. Tuache kulalamika sana kwa kuwa ukiwa mlalamishi sana, unapoteza utulivu wa kukupeleka katika njia sahihi ya kufanya kinachotakiwa katika wakati mwafaka. Kubali makosa, jifunze na uwe wewe mpya.

KIMENUKA TENA! MAPACHA WA P-SQUARE KUBURUZANA MAHAKAMANI

0


Wasanii maarufu nchini Nigeria, ambao ni mapacha Peter na Paul Okoye (P-Square) huenda wakaburuzana mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuwa Paul ametumia picha ya mwenzake kwenye tangazo la tamasha lake nchini Angola.

Peter ambaye ni mlalamikaji, amesema kuwa anatarajia kwenda mahakamani kumshtaki ndugu yake, Paul kwa kutumia picha zake kwa ajili ya kutangaza tamasha hilo la muziki.

“Kwahiyo wameamua kutumia picha yangu ili wauze tiketi za show yao huko Angola. “Nyie mapromota na uongozi mzima, mwanasheria wangu atalifuatilia suala hilo mapema iwezekanavyo,” ameandika Peter kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, tayari Paul Okoye ameshafanya shoo yake juzi Jumapili Mei 26, 2019, usiku nchini Angola.

Peter na Paul ni mapacha na zamani waliunda kundi la P-Square ambalo lilipata umaarufu zaidi duniani kupitia nyimbo kadha wa kadha ikiwemo Personally, Temptation na nyinginezo.

Kwa sasa kundi hilo limevunjika kwa sababu mbalimbali ikiwemo za maslahi binafasi na kifamilia, japo kumekuwa na masuluhisho kadhaa ya kurudisha kundi hilo.

SIMBA FULL SHANGWE LEO WABEBA KOMBE LAO LA 20 TPL

0


MABINGWA watetezi Simba leo wamekabidhiwa kombe la Ligi Kuu Bara na mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola baada ya kumaliza mchezo wao wa mwisho uliochezwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Kwenye mchezo wa leo, Mtibwa Sugar wamelazimisha suluhu ya kutofungana wakiwa nyumbani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Uhuru.

Huu ni ubingwa wa 20 kwa Simba wakiwa nyuma ya wapinzani wao wa karibu Yanga ambao wamebeba ubingwa huo mara 27.

Kesho watarejea Dar na kombe hilo huku sherehe zikianzia maeneo ya Kibaha ambapo wachezaji watapanda kwenye gari la wazi wakionyesha kombe walilotwaa  msimu wa mwaka 2018/19 baada ya kufikisha jumla ya pointi 93 wakiwa nafasi ya kwanza.

Stand United yashuka rasmi daraja!

0

Timu ambayo ilikuwa inasubiriwa kushuka daraja kuungana na African Lyon imepatikana rasmi. Stand United ya Shinyanga rasmi wameshuka daraja baada ya kufungwa na JKT Tanzania kwa goli 2-0 na JKT Tanzania.

Timu mbili ambazo zitacheza playoff (Michezo ya mitoano ) ni Kagera Sugar aliyeshika nafasi ya 18 na Mwadui FC aliyeshika nafasi ya 17.

Mwadui na Kagera watacheza na Pamba FC ya Mwanza na Geita Sports ya Geita. Mshindi wa playoff atapanda ligi kuu Tanzania bara msimu ujao tena

# Timu P W D L GD Pts
1 Simba SCSimba SC 38 29 6 3 62 93
2 Yanga SC 38 27 5 6 29 86
3 Azam FC 38 21 12 5 33 75
4 KMC FC 38 13 16 9 15 55
5 Mtibwa Sugar FC 38 14 8 16 1 50
6 Lipuli FC 38 12 13 13 -8 49
7 Mbeya City FC 38 13 9 16 -1 48
8 Coastal Union FC 38 11 15 12 -10 48
9 Ndanda FC 38 12 12 14 -12 48
10 JKT Tanzania SC 38 11 14 13 -6 47

The post Stand United yashuka rasmi daraja! appeared first on Kandanda.

329,001FansLike
12,344FollowersFollow
16,900SubscribersSubscribe

EDITOR PICKS