Tuesday, January 13, 2026
Home Blog Page 2953

Mechi yetu na Azam FC ilikuwa ya kirafiki- Zahera

0

 

Jana katika uwanja wa Taifa kulikuwa na mechi kati ya Yanga na Azam FC, mechi iliyomalizika kwa Azam FC kushinda goli 2-0.

Baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Yanga amedai kuwa mechi hiyo ilikuwa ni kama ya kirafiki kwa sababu wachezaji walikuwa wanacheza wanavyojisikia.

” Mechi haikuwa na ushindani, wachezaji walikuwa wanacheza bila maelekezo. Unaona Makambo anabaki na kipa lakini hakuna anachokifanya”.

Alisema kocha huyo ambaye amewezesha timu hii kushika nafasi ya pili licha ya matatizo mengi ya timu yake ya Yanga.

The post Mechi yetu na Azam FC ilikuwa ya kirafiki- Zahera appeared first on Kandanda.

Okwi sio mchezaji wa Simba! Kaizer Chiefs yahusika

0

Juzi Emmanuel Okwi aliandika katika mtandao wake wa Instagram kuwa neno kwa heri ni neno chungu sana.

Maneno ambayo yaliweka mjadala kuhusiana na Emmanuel Okwi kuendelea kuwepo Simba. Leo hii Simba imedhibitisha kuwa Emmanuel Okwi siyo mchezaji wao.

Akizungumza na mtandao huu , mkuregenzi mtendaji wa Simba, bwana Magori amedai kuwa Emmanuel Okwi ameshamaliza mkataba na Simba.

Alipoulizwa kuhusu tetesi za Emmanuel Okwi kutakiwa na Kaizer Chiefs ya Afrika kusini amedai kuwa hana hizo taarifa hizo.

“Hizo habari hata Mimi sizijui kama wewe, labda uzungumze na mchezaji mwenyewe ambaye kashamaliza mkataba na Simba”.

” Sijapata hiyo barua, ninachojua Emmanuel Okwi alimaliza mkataba, tukakaa naye akaomba aende kwanza Afcon na akitoka tuendelee na mazungumzo naye”.

“Na mpaka sasa hivi kwenye mikono yake amedai kuwa ana ofa tatu mpaka sasa hivi, hivo tumemwacha aende Afcon, akirudi tutazungumza naye”.Alimaliza kuongea mkurugenzi huyo mtendaji wa Simba

The post Okwi sio mchezaji wa Simba! Kaizer Chiefs yahusika appeared first on Kandanda.

RUVU SHOOTING HAWAAMINI WANACHOKIONA TPL

0


KOCHA wa Ruvu Shooting, Ablumutik Haji amesema kuwa haamini macho yake kubaki ligi kuu kwani alikuwa anapitia kipindi kigumu msimu huu hali iliyomfanya akate tamaa.

Ruvu Shooting jana ilishinda mbele ya Alliance kwa bao 1-0 na kubaki kwenye ligi baada ya kufikisha jumla ya pointi 45 ikiwa nafasi ya 15.

“Ngumu kuamini ila mwisho wa siku namshukuru Mungu kwa kutupigania na kutupa nafasi nyingine msimu mwingine, tutapambana kwa hali na mali maana msimu huu haukuwa bora kwetu,” amesema.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO

0
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele Gazeti la CHAMPIONI Jumatano


YANGA YATAJA KILICHOIPONZA KUKOSA UBINGWA MSIMU HUU

0


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa T-Shirti lake alilokuwa analipenda kuvaa msimu huu halina bahati ya kubeba ubingwa hivyo msimu ujao atabadilisha ili abebe ubingwa.

Yanga jana wamepoteza mchezo wao wa mwisho mbele ya Azam FC kwa kufungwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.

Zahera amesema kuwa sababu kubwa ya kuvaa T.Shirt hiyo ni nembo yake ambayo ameiteua msimu huu.

“Kila mmoja ana mtindo wake unaomtambulisha hivyo kwangu mimi T.shirt yangu ni utambulisho wangu pamoja na hii kofia, ila sasa nimeona haikuwa na bahati msimu ujao nitaboresha zaidi.

“Tumefungwa kwa kuwa wachezaji hawakuwa na morali kubwa ila hakukuwa na chochote cha kupoteza ila ni matokeo tu yametokea tumepoteza,” amesema Zahera.

SIMBA: HAIKUWA RAHISI KUFIKA HAPA

0


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kwao kutwaa ubingwa kwani walicheza mfululizo hasa kipindi cha mwisho ila juhud zimewapa walichokuwa wanastahili.

Aussems amesema kuwa wachezaji wake walikuwa wamechoka kutokana na kucheza michezo 15 ndani ya siku 30 ila hawakuwa na jinsi zaidi ya kutafuta matokeo.

“Haikuwa safari nyepesi kufika hapa, tumecheza michezo mingi ile ya karibu ikiwa ni 15 ndani ya siku 30 ni ngumu sana kupata matokeo chanya muda wote.

“Kwa upande wa waamuzi muda wote nimekuwa nikiona wakifanya majukumu yao ila sikupaswa kujali kwa kuwa wanatimiza majukumu yao ingawa kuna wakati walikuwa wanafanya maamuzi ambayo yanatuumiza sisi pamoja na wapinzani wetu,” amesema.

MUONEKANO WA GAZETI LA CHAMPIONI KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMATANO

0


MUONEKANO WA GAZETI LA CHAMPIONI KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMATANO

YANGA YAFUNGUKA JUU YA KUMSAJILI NDEMLA

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kumsajili kiungo wa Simba, Said Ndemla ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na kikosi chake.

Zahera amesema kuwa mpango wake ni kuwa na kikosi bora ambacho kitakuwa na ushindani msimu ujao kutokana na aina ya wachezaji ambao anawataka.

“Sina mpango wa kumsajili Said Ndemla, simjui huyo mchezaji na hayupo kabisa kwenye hesabu zangu.

“Nataka kufanya usajili ambao utakuwa na tija hivyo mashabiki wa Yanga watulie wasiwe na presha kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.

NDUGU YAKE NA MEDDIE KAGERE AMWAGA WINO YANGA

0


Imefahamika kuwa winga hatari wa kulia na kushoto anayekipiga Klabu ya Mukura Victory Sports ya Rwanda, Patrick Sibomana, usiku wa kuamkia juzi alipanda ndege ya Rwand Air na kutua nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Yanga.

Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera aliwahi kuliambia Gazeti la Championi kuwa yupo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji sita wa kimataifa watakaokuja kuichezea timu hiyo kutoka Rwanda, Nigeria, Ivory Coast na Guinea.

Hiyo yote ni katika kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga imepania kuuchukua ubingwa.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti la Championi limezipata zinasema kuwa winga huyo amekuja kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kupewa mkataba wa kuichezea timu hiyo.

“Muda mrefu Yanga walikuwa wanamuwania winga huyo tangu msimu uliopita, baada ya kushindikana kukamilisha usajili wake.

“Lakini msimu huu wamepanga kumsajili katika kukamilisha ripoti ya kocha aliyoitoa ya kukamilisha usajili wa kila mchezaji anayemuhitaji katika kuelekea msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela, alipotafutwa kuzungumzia hilo, alisema: “Siwezi kukubali au kukataa ujio wa winga huyo, ukweli wapo wachezaji wengi wanaotarajiwa kutua nchini kwa ajili ya kusajiliwa, hivyo tusubirie suala hilo kama likikamilika tutaweza wazi.”

Jana jioni Championi lilimshuhudia winga huyo akiwa hoteli moja jijini Dar na viongozi wa Yanga akiwemo Mwakalebela na Samuel Lukumay wakifanya mazungumzo ya kumpa mkataba ambao unaaminika ni wa miaka miwili.

Sibomana ametua Dar es Salaam akitokea Rwanda likiwa ni taifa moja analotokea straika hatari wa Simba, Meddie Kagere.

ZAHERA: NITAWAFUKUZA WACHEZAJI WOTE – VIDEO

0


TIMU ya Azam FC jana Jumanne, Mei 28, 2019 wamelipa kisasi baada ya kuifunga Yanga Sc kwa mabao 2-0, mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania bara uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

SIKILIZA ALICHOKIZUNGUMZA ZAHERA HAPA KUHUSIANA NA WACHEZAJI YANGA


329,001FansLike
12,344FollowersFollow
16,900SubscribersSubscribe

EDITOR PICKS