Home Uncategorized BAADA YA KUTWAA KOMBE, HAZARD KUSEPA CHELSEA

BAADA YA KUTWAA KOMBE, HAZARD KUSEPA CHELSEA


Eden Hazard, baada ya kutimiza jukumu lake ndani ya kikosi hicho kutwaa kombe la Europa League kwa kuifunga Arsenal mabao 4-1, amesema kuwa anataka kwenda Real Madrid. 
Hazard alifunga mabao 2 kati ya mabao 4-1 ambayo wameshinda mbele ya Arsenal na kutwaa kombe ikiwa ni mara ya kwanza kutwaa taji hilo mbele ya Meneja wao Maurizio Sarri.
Baada ya mchezo kuisha, Hazard amethibitisha kuiacha klabu hiyo ya darajani na kujiunga na klabu ya Real Madrid msimu ujao kwa dau la Euro milioni 115.
“Nimeshafanya maamuzi yangu tayari, niliweka wazi wiki mbili zilizopita, sasa ni kazi kwa timu yangu yenyewe na timu nyingine ambayo ninataka kwenda, kwa sasa ninasubiri kama ambavyo mashabiki wanasubiri, tutajua kuhusu hili baada ya muda
“Nafikiria kusema kwa heri kwa kuwa kwenye mpira huwezi kujua, ndoto zangu zilikuwa ni kucheza Ligi Kuu ya England, jambo hilo nimelifanya kwa muda wa miaka saba sasa ni muda wa kupata changamoto mpya,” amesema.
SOMA NA HII  LEO NI VITA YA TANO BORA ENGLAND, BRUNO NOMA