Home Uncategorized Walcot asajiliwa Yanga.

Walcot asajiliwa Yanga.

Harakati za usajili wa Yanga zinaendelea kwa kasi kwa ajili ya kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao , baada ya kuteseka sana msimu huu.

Imedhibitishwa rasmi kuwa Yanga imemsajili kiungo wa APR, Issa Birigimana ambaye huitwa Theo Walcot na mashabiki kutokana na aina ya uchezaji wake kufanana na Theo Walcot.

Issa Birigimana amedhibitisha yeye mwenyewe kuwa msimu ujao atakuwa mchezaji rasmi wa Yanga kwa msimu ujao.

“Tayari nimesaini kabisa mkataba na Yanga. Nimesaini mkataba wa miaka miwili (2) kwa hiyo nawaahidi mashabiki wa Yanga nilichokuwa nakifanya APR nitakifanya zaidi nikiwa na Yanga”- alidai mchezaji huyo alipokuwa anazungumza na kituo cha Radio cha EFM.

The post Walcot asajiliwa Yanga. appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  KUHUSU KIWANGO CHAKE KUSHUKA..KICHUYA AMEFUNGUKA HAYA..!!