Home Uncategorized LIPULI FC, KOCHA WAO MATOLA BADO HAKIJAELEWEKA KIANA

LIPULI FC, KOCHA WAO MATOLA BADO HAKIJAELEWEKA KIANA


Uongozi wa Lipuli FC umesema kuwa bado haujakaa mezani kuzungumza na kocha, Seleman Matola juu ya kuongeza mkataba mpya kwa ajili ya msimu ujao.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Ofisa Habari wa Lipuli, Clement Sanga amesema kuwa baada ya ligi kuisha na kumaliza mchezo wa fainai kombe la Shirikisho walimpa mapumziko kocha pamoja na wachezaji.

“Kwa sasa bado hatujazungumza na kocha wetu Matola kwa kuwa baada ya kumaliza ligi pamoja na mchezo wetu wa FA tulimpa mapumziko hivyo muda ukikamilika tutamuita mezani kuyajenga.

“Amekuwa mwalimu bora ambaye msimu huu ametufanyia makubwa tunamheshimu na tunamuamini, kikubwa ninachojua bado ni mali yetu kwa kuwa hakuna taarifa mpya ambazo tumezipata juu yake licha ya kwamba tunajua lazima atakuwa anapigiwa mahesabu na timu nyingine,” amesema Sanga.

SOMA NA HII  KASI YA NYOTA MPYA WA SIMBA YAMKOSHA MBELGIJI WA SIMBA, ALICHOKIFANYA DAKIKA 12 NI BALAA