Home Uncategorized HAWA HAPA 11 WANATAJWA KUVAA JEZI YA SIMBA MSIMU UJAO

HAWA HAPA 11 WANATAJWA KUVAA JEZI YA SIMBA MSIMU UJAO


IMEELEZWA kuwa kikosi cha Simba kinafanya kazi ya usajili kimyakimya ambapo mpaka sasa hakijatangaza mchezaji hata mmoja ambaye amesajiliwa hata kwa mkataba wa awali.

Habari zimeeleza kuwa mpaka sasa Simba wanapitia ripoti iliyoachwa mezani na kocha mkuu, Patrick Aussems ambaye yupo likizo nchini Ubelgiji kwa sasa.

Hii hapa ni orodha ya baadhi ya wachezaji ambao inasemekana wanahitajika ndani ya kikosi hicho kinachojiandaa kwenda kuweka kambi nje ya nchi mwezi Julai baada ya michuano ya Afcon kukamilika kwa muda wa wiki sita:-

Bangala Litombo anayekipiga  AS Vita ya Congo.

Walter Bwalya anaitumikia Nkana Fc ya Zambia.


Francis Kahata anaitumikia klabu ya Gor Mahia ya Kenya.


Chilunda kwa sasa ni mchezaji huru yupo na timu ya Taifa ya Tanzania inayokwea pipa kuelekea Misri.

Ibrahim Ajibu ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga.


Beno Kakolanya ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na Yanga.

Kassim Khamis, anakipiga pale Kagera Sugar aliitwa timu ya Taifa leo ameachwa.

Haruna Shamte anaitumikia timu ya Libuli.

Idd Naldo anaitumikia timu ya Mbeya City.

Salum Kimenya, yupo kwa wanajelajela,Tanzania Prisons. 

Dickson Ambundo wa Alliance.

SOMA NA HII  POLISI TANZANIA YAMALIZANA NA NYOTA WATATU KWA MPIGO,MMOJA ALIKUWA ANAKIPIGA KMC