Home Uncategorized KESI YA AVEVA, KABURU, HANSPOPE YAKWAMA LEO

KESI YA AVEVA, KABURU, HANSPOPE YAKWAMA LEO

Habari za Simba leo


Kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa  Simba imeshindwa kuendelea kusikilizwa baada ya shahidi aliyeandaliwa  kufiwa na kushindwa kufika mahakamani.

Kesi hiyo inawakabili  hao waliokuwa viongozi wa Simba Evans Aveva na Godfrey Nyange ‘Kaburu’  ambao wanakabiliwa na shitaka la kughushi na kutakatisha  fedha huku Zachariah Hans Pope akiunganishwa katika kesi hiyo yeye kwa kudaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo za ununuzi wa nyasi bandia.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea leo Jumatatu kwa kusikilizwa ushahidi wa shahidi wa tano.

Wakili wa Serikali, Leonard Swai aliiambia mahakama kuwa tayari alikuwa ameandaa shahidi lakini alimpigia simu kuwa amefiwa mkewe hivyo ameshindwa kufika.

Hivyo Swai aliiomba mahakama kupangiwa tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kesi hiyo.

Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba alisema upande wa serikali uhakikishe kuwa unaanda mashihidi  watatu ili akikosekana mmoja awekwe mwingine.

Swai ametakiwa kuleta mashahidi wengi watatu katika kesi hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea  Juni 12 na 13 mwaka huu.

SOMA NA HII  MSOLLA: SIJAFIKIRIA KUJIUZULU YANGA