Home Uncategorized Kiungo wa Simba amwaga wino Namungo fc

Kiungo wa Simba amwaga wino Namungo fc

Kiungo mshambuliaji John Mbise amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili kutumikia Wana wa Ruhangwa ya Lindi baada ya kuipandisha Ligi Kuu.

John Mbisse aliepitia Simba kati ya mwaka 2014 na 2016 akiwa katika kikosi cha kina Mbaraka Yusuph, Idd Kipagwile, Issa Ngoa na Denis Richard.

Baada ya kumwaga wino John Mbise alisema “Ni furaha kuendelea kubaki Namungo tena, ni wakati mwingine tena wa kuipigania timu ibaki Ligi Kuu kama tulivyoipandisha”

Mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo wa kukaba na kushambulia amefunga goli moja huku pia akitoa pasi tatu zaa mabao katika harakati za kuipandisha Namungo fc aliyojiunga nayo dirisha dogo akitokea Friends Rangers.

John Mbise pia amepitia vilabu mbalimbali kama Mshikamano fc, Dodoma fc na Friends Rangers kwa nyakati tofauti.

The post Kiungo wa Simba amwaga wino Namungo fc appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  KAZE ATANGAZA HALI YA HATARI YANGA