Home Uncategorized MBALI NA BOCCO, POLOKWANE WAMTAKA MWINGINE SIMBA

MBALI NA BOCCO, POLOKWANE WAMTAKA MWINGINE SIMBA


KLABU ya Polokwane ya Afrika Kusini imekubali yaishe kwa mshambuliaji wa Simba, John Bocco na kumuomba kwa mkopo Adam Salamba aende kukipiga nchini huko.

Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu utata uibuke mara baada ya picha Bocco kusambaa zikimuonyesha akisaini mkataba mwingine wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo na Polokwane kuibuka na kudai ni mshambuliaji ni mali yao baada ya kumsainisha mkataba wa awali.

Bocco ni kati ya wachezaji walioongeza mikataba hivi karibuni baada ya awali kumalizika wengine ni Erasto Nyoni, Aishi Manula na Jonas Mkude aliyeondolewa kwenye mchujo wa awali wa Timu ya Taifa, Taifa Stars.

Akizungumza na Championi Juma mosi, Mtendaji Mkuu wa Simba Sports Company Limited, Cresencentius Magori alisema suala la utata kuhusu usajili wa Bocco na Polokwane limemalizika baada ya kuona walifanya makosa na juzi walimuomba mchezaji wao Salamba aende akaichezee kwa mkopo.

Magori alisema kuwa suala hilo lipo mezani kwao bado uongozi haujaamua kumuachia mshambuliaji huyo aende huko, lakini hivi karibuni itajulikana baada ya kujadiliana na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbelgiji, Patrick Aussems.

“Limekwisha hilo suala la utata wa Bocco na Polokwane, na uzuri wenyewe wamekiri kufanya makosa katika usajili wake wa kumsajili akiwa bado ana mkataba na ni makosa kisheria kwa mujibu wa kanuni za Fifa.

“Katika kuthibitisha hilo, hao Polokwane wamemuomba mchezaji wetu (Salamba) ili aende akaiongezee nguvu safu ya ushambuliaji yao na kama mambo yakienda vizuri basi atakwenda huko kucheza soka la kulipwa.

“Pia, ilikuwa ngumu kwa Bocco kwenda kucheza soka huko Polokwane, labda sababu ya Afrika Kusini lakini siyo kwa ajili ya malengo, Simba ni klabu kubwa Afrika,” alisema Magori.

SOMA NA HII  NYOTA YANGA AGOMBANIWA NA TIMU ZA LIGI KUU BARA ZIKITAKA SAINI YAKE