Home Uncategorized SALAMBA AAMUA KUFUNGUKA, ATOA MSIMAMO WAKE SIMBA

SALAMBA AAMUA KUFUNGUKA, ATOA MSIMAMO WAKE SIMBA


Mshambuliaji wa Simba, Adam Salamba atabakia klabuni hapo kwa msimu ujao endapo kocha wake Patrick Aussems atamhitaji. Ingawa kwa hali ilivyo ni asilimia ndogo.

Salamba amekuwa akitajwa kuwa moja ya wachezaji ambao wanawezwa kuachwa.

Salamba amesema kuwa kusalia ama kutosalia ndani ya Simba msimu ujao hilo litabakia kwa Kocha wake.

“Hilo la kubakia ndani ya timu kwa msimu ujao ni masuala ya mwalimu siyo mimi.

“Akitaka nitaendelea kubakia hapa na kama akiamua nisiendelee basi nitajua la kufanya.”

SOMA NA HII  YANGA SASA NI BALAA, SIBOMANA AMWAGA WINO WA MIAKA MIWILI YANGA