Home Uncategorized AJIBU AKATAA JEZI SIMBA

AJIBU AKATAA JEZI SIMBA


AJIBU ameliamsha Msimbazi baada ya kugomea kukabidhiwa jezi namba 23.

Namba hiyo 23 ilikuwa inavaliwa na kiungo huyo mtaalam wa assisti, awali akiwa anaichezea Simba kabla ya kutua Yanga msimu wa 2017/2018 kama mchezaji huru.

Inasemekana kuwa, Ajibu alishasaini mkataba wa miaka miwili muda mrefu kabla ya kutambulishwa jana wakati wa lanchi baada ya mkataba wake kumalizika rasmi juzi Jumatatu.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Ajibu amewaambia mabosi wa timu hiyo kuwa yeye ni staa hivi sasa na jezi anayotaka ni namba 10 na siyo 23.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, mabosi hao wamepanga kumpatia jezi hiyo namba 10 anayoitaka ambayo hivi sasa haivaliwi na mchezaji yeyote baada ya aliyekuwa anaivaa, Adam Salamba kwenda kucheza soka la kulipwa Sauzi.

Alipotafutwa Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu kuzungumzia hilo alisema kuwa “Ndiyo kwanza tunamalizia mapumziko yetu, hivyo hilo zoezi la jezi bado halijaanza kugawiwa kwa wachezaji.”

SOMA NA HII  BUNDESLIGA YAREJEA KWA KISHINDO, HAALAD AANZA YAKE