Home Uncategorized AZAM FC WAFICHUA SIRI KUWANG’OA TP MAZEMBE KAGAME

AZAM FC WAFICHUA SIRI KUWANG’OA TP MAZEMBE KAGAME

ETTIENE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC, amesema kuwa siri kubwa ya timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kagame ni ukubwa wa timu kwenye michuano hiyo.


Azam FC ilishinda kwa mabao 2-1 mchezo wa hatua ya robo fainali na mabao ya Azam FC yalipachikwa na Iddy Naldo pamoja na Obrey Chirwa.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ndayiragije amesema kuwa aliwaambia wachezaji wajiamini na wanaweza kufanya makubwa mbele ya TP Mazembe.

“Niliwaambia wachezaji wasiwe na mashaka, uwezo mkubwa wanao na sisi ni timu kubwa kutokana na kuwa mabingwa watetezi wa kombe, hivyo hicho kimetubeba,” amesema Ndayiragije.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amewashukuru watanzania kwa sapoti zao na dua kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo baada ya KMC kuondolewa.
SOMA NA HII  KOSI KAZI LA NYOTA WA MTIBWA SUGAR ANAYEWINDWA NA YANGA LIPO NAMNA HII