Home Uncategorized DUH! BARCELONA WAMFUNGIA VIOO NEYMAR JUMLAJUMLA

DUH! BARCELONA WAMFUNGIA VIOO NEYMAR JUMLAJUMLA

JOSEP Bartomeu Rais wa Barcelona amesema kuwa klabu yake haina mpango wa kujaribu kupata saini ya kumpata mchezaji Neymar JR kwani Paris Saint Germain hawana mpango wa kumuuza.
“Najua kwamba Neymar anahitaji kurejea ndani ya kikosi cha Barcelona akitokea PSG lakini tunajua kwamba timu yake haiwezi kumruhusu arejee ndani ya kikosi chetu,” amesema.
Maneno haya yamemvunja moyo nyota huyo anayekipiga PSG kwani tayari ameshajua kwamba hana nafasi tena ndani ya kikosi hicho ambacho alicheza zamani.
SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA LEO DHIDI YA KAGERA SUGAR