Home Uncategorized GADIEL MICHAEL: NASAINI SIMBA JUMLA

GADIEL MICHAEL: NASAINI SIMBA JUMLA

IMEELEZWA kuwa beki wa Yanga, Gadiel Michael amemalizana na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kukitumikia kikosi hicho msimu ujao.

Michael alipishana na Yanga kutokana na kumuwekea dau dogo jambo ambalo limemfanya aamue kujiunga na Simba ili kumfuata rafikiye wa karibu Ibrahim Ajibu.

Chanzo cha kuaminika kimeeleza kwamba tayari Gadiel amemalizana na Simba hivyo anachosubiri kwa sasa ni kutambulishwa.

“Tayari Gadiel amemalizana na Simba na amesaini kandarasi ya miaka miwili, amefanya hivyo baada ya kuwekewa dau kubwa tofauti na lile alilowekewa Yanga,”kilieleza chanzo hicho.

Gadiel Michael mwenyewe amesema kuwa hana tatizo kumwaga wino ndani ya Simba kwani yeye ni mchezaji hachagui kambi.

“Hakuna tatizo kwa mimi kusaini Simba kwani mchezaji hachagui kambi, hivyo kama Yanga nimeshindwana nao sioni taabu kusaini Simba, na itafahimika muda si mrefu kuwa nimesaini Simba,” amesema Gadiel.

SOMA NA HII  YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA JKT TANZANIA