Home Uncategorized IMEVUJA!! KABWILI ALISHAPATA OFA MACEDONIA AKILIPIWA KILA KITU, MPAKA SASA YUPO MORO

IMEVUJA!! KABWILI ALISHAPATA OFA MACEDONIA AKILIPIWA KILA KITU, MPAKA SASA YUPO MORO


Imeripotiwa kuwa hivi karibuni ilisema kuwa klabu ya FK Renova ya Macedonia barani ulaya ilimpa ofa golikipa wa klabu ya Yanga, Ramadhani Kabwili ya kwenda kufanya majaribio ya wiki mbili.

Ofa hiyo ilitakiwa kuanza kwa majaribio June 24 na ikielezwa kuwa klabu hiyo itamgharamikia nauli ya ndege, chakula na malazi kwa wiki zote mbili ambazo atakuwa huko.

Licha ya ofa hiyo kutumwa, mpaka sasa Kabwili yupo Tanzania akiwa kambini Morogoro na klabu ya Yanga.

Haijajulikana mpaka sasa hatma ya suala lake limekaaje ingawa katika orodha ya majina ya Yanga yaliyopelekwa CAF jina lake halipo.

Ikumbukwe mkataba wa Kabwili na Yanga mpaka sasa umeshamalizika na yupo huru kuelekea pengine kusaka maisha.

SOMA NA HII  MBIVU NA MBICHI ZA ZITAKAZOSHUKA NA KUPANDA TPL KUJULIKANA LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here