Home Uncategorized KAGERA SUGAR YAMVUTIA KASI MUIVORY COAST KUMRITHI KASSIM KHAMIS

KAGERA SUGAR YAMVUTIA KASI MUIVORY COAST KUMRITHI KASSIM KHAMIS

WILLFRED Kouroma mshambuliaji wa Biashara United raia wa Ivory Coast ameingia kwenye rada za uongozi wa Kagera Sugar ambao wanaimarisha kikosi.

Inaelezwa kuwa Kagera Sugar wanahitaji huduma ya Kouruma ambaye ataziba pengo la Kassim Khamis ambaye ametimkia Azam FC.

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa kazi kubwa kwa msimu ujao ni kuleta ushindani msimu ujao.

“Hesabu zetu ni kuona msimu ujao tunaleta ushindani hivyo usajili wetu lazima uwe makini, kuhusu huyo nyota wa Biashara bado hatujakamilisha mipango ikikamilika tutaweka wazi,” amesema.

SOMA NA HII  SABABU YA RUVU SHOOTING KUFANYA KLINIKI KWA WACHEZAJI YATAJWA