Home Uncategorized KOCHA STARS: TUPO TAYARI KUPAMBANA NA KENYA

KOCHA STARS: TUPO TAYARI KUPAMBANA NA KENYA

ETTIENE Ndayiragije, Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa imani ni kubwa kwa timu ya Taifa ya Tanzania kupata matokeo chanya mbele ya timu ya Kenya kwenye michuano ya Chan.

Tanzania itacheza kesho na Taifa Stars uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Chan.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ndayiragije amesema kuwa kikosi kinazidi kuimarika na wachezaji wana morali kubwa ya kufanya vizuri.

“Mpaka sasa tupo sehemu nzuri, tumeanza na kuwajenga wachezaji kisaikolojia na kujenga muunganiko mzuri kwa timu.

“Hautakuwa mchezo mwepesi ila tumejipanga kufanya vizuri hivyo mashabiki muda wao ni sasa kutupa sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA YAGOMA KUSHUKA NAFASI YA KWANZA NDANI YA LIGI KUU BARA