Home Uncategorized MBARAZIL WA SIMBA AKIWASHA HUKO SAUZI

MBARAZIL WA SIMBA AKIWASHA HUKO SAUZI

MBRAZIL anayekipiga Simba ambaye ni kiraka anacheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji Gerson Vieira amesema kuwa ni furaha kuwa ndani ya Simba kwa sasa.

Vieira  amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya kikosi cha Simba kwenye usajili wa dirisha kubwa akitokea timu ya ATK FC ya India kwa sasa yupo na timu nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Mbrazil huyo amesema :”Wachezaji wenzangu walinipokea vizuri jambo linalonipa furaha na ninafurahi kuwandani ya Simba.

“Tupo na Kocha mwenye uwezo mkubwa hivyo tunaamini tutafanya makubwa pia na kila mmoja yupo vizuri, na tuna kocha mwenye uwezo mkubwa,” amesema.

SOMA NA HII  BERNARD MORRISON ASHANGAZWA NA MASHABIKI WA YANGA