Home Uncategorized Metacha ni nyanda anayekuja kusahihisha makosa ya Manula

Metacha ni nyanda anayekuja kusahihisha makosa ya Manula

 

KAMA kweli atakamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga SC akitokea Mbao FC, golikipa, Metacha Mnacha atakuwa bora Zaidi ya Aishi Manula na atashikilia namba moja ya timu ya Taifa. Licha ya klabu yake ya Mbao FC kupigania kutoshuka daraja hadi siku ya mwisho ya msimu uliopita, Mnacha aliweza kuonyesha uwezo wake wa kuzuia akiwa golini.

Wakati, Aishi akionekana kufanya makossa mengi kiuchezaji, Mmnacha anaweza kuja kutukumbusha baadhi ya ‘Tanzania One’ waliopita nchini. Akiwa na kimo kirefu, umbo pana kiasi na mikono mirefu Zaidi ya ‘Tanzania One wa Mwisho’ na wa kwanza wa karne mpya Juma Kaseja, Mnacha anaweza kusahihisha baadhi ya makossa muhimu katika lango la timu ya Taifa.

i
Kujiunga kwake na Yanga kunamaanisha atakuwa amekubali vita ya magolikipa watatu- Mkenya, Farouk Shikalo na kijana Ramadhani Kabwili. Akiwa tayari ameonyesha uwezo mkubwa wa kucheza ‘mipira ya wazi’, kasi nzuri katika kutokea na uwezo wa kuliziba goli lake, Mnacha anaweza kuwa kipa namba moja katika timu ya Taifa kama tu atafanikiwa kuishika namba moja ya Yanga.

Manula amekuwa akifanya makossa mengi na kuhusika katika baadhi ya magoli muhimu ya timu pinzani. Uwezo wa kucheza krosi, na mikwaju ya mbali kwa kipa huyo namba moja wa Simba SC na timu ya Taifa siku zote unatia shaka.

Licha ya kucheza vizuri kwa muda mwingi wa mchezo dhidi ya Kenya, Manula alihusika na magoli mawili kama si yote matatu yaliyofungwa na Kenya katika mchezo wa pili kwa Stars katika michuano ya Mataifa ya Afrika ambayo tayari wameondolewa katika michuano hiyo.

Mnacha alipewa nafasi ya kuichezea Taifa Stars kwa mara ya kwanza na licha ya kuruhusu magoli matatu dhidi ya Algeria kwa mchezaji kijana kama yeye kucheza mchezo wa kwanza wa timu ya Taifa ukiwa katika michuano mikubwa Zaidi ya kimataifa barani Afrika ni ishara nzuri, na kama atafanikiwa kuonyesha kiwango cha juu katika michezo miwili ijayo ya Taifa Stars dhidi ya Kenya katika kuwania kufuzu kwa CHAN, nyanda huyo atakuwa karibu kabisa kumpora nafasi ya kuanza katika kikosi cha timu ya Taifa Stars, Aishi.

SOMA NA HII  HUU HAPA MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA

Yanga ni klabu kubwa Zaidi katika soka la Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki, hivyo Mnacha kama anataka kufanikiwa kufikia malengo yake makubwa anapaswa kila wakati kuwa tayari kusahihisha makossa, anatakiwa kujituma Zaidi katika viwanja vya mazoezi, na kuwa tayari kushipigania nafasi.

Akiwa tayari ameonyesha uwezo mzuri kiasi cha kushinda tuzo ya golikipa bora wa michuano ya SportsPesa Super Cup mapema mwaka huu-mtaalam huyo wa kucheza mikwaju ya penalty anaweza kutusahihishia baadhi ya makossa muhimu yanayofanywa na Manula na pia atatukumbusha kizazi kile cha mwisho cha Tanzania One-Yanga ndiyo ngazi yake sahihi.

The post Metacha ni nyanda anayekuja kusahihisha makosa ya Manula appeared first on Kandanda.