Home Uncategorized NAHODHA STARS: WALILAZIMISHA SARE KWETU NASI TUNAKWENDA KUSHINDA KWAO

NAHODHA STARS: WALILAZIMISHA SARE KWETU NASI TUNAKWENDA KUSHINDA KWAO

JUMA Kaseja, nahodha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa nafasi ya kushinda kwa timu nchini Kenya ipo kikubwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki.

Taifa Stars mchezo wa kwanza wa kufuzu michuano ya Chan inayotarajiwa kufanyika Cameroon 2020 ililazimisha suluhu ya bila kufungana dhidi ya Kenya uwanja wa Taifa mchezo wa marudio utakuwa Agosti 4 nchini Kenya.

Kaseja amesema : “Wao wameweza kupata sare kwenye ardhi ya nyumbani, basi nasi tunaweza kupata ushindi kwenye ardhi yao Kenya, makosa yetu benchi la ufundi litafanyia kazi nasi tunajipanga tukiaimini tuna nafasi ya kusonga mbele.

“Morali kwa wachezaji ni kubwa na kila mmoja anatambua kazi yake, kikubwa ni sapoti kwa mashabiki na dua,” amesema.

SOMA NA HII  AZAM FC: TUNAFANYIA KAZI MAPUNGUFU YETU KWA MICHUANO YA KIMATAIFA