Home Uncategorized NAMUNGO FC YAFANYA BIASHARA NA BAROLA WA BIASHARA UNITED

NAMUNGO FC YAFANYA BIASHARA NA BAROLA WA BIASHARA UNITED


NURDINE Barola aliyekuwa mlinda mlango wa kikosi cha Biashara United amesajiliwa na timu ya Namungo FC kwa kandarasi ya mwaka mmoja.

Barola alifanya kazi na Kocha Mkuu wa Namungo FC, Hitimana Thiery kabla ya kutimuliwa ndani ya kikosi cha Biashara.

Anaungana na bosi wake wa zamani ambaye ndiye aliipandisha Namungo FC kwenye Ligi Kuu Bara kutoka Ligi Daraja la Kwanza.

SOMA NA HII  SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU JONAS MKUDE